Habari za Punde

Samsung Yazindua Simu ya Samsung Galaxy S7.

 Balozi wa Samsung Tanzania,Aisha Saki(katikati) akiwaelezea jambo wateja waliotembelea uzinduzi wa simu ya Samsung Galaxy S7 Mlimani City jijini Dar es Salaam.Kulia ni mabalozi na wenzake. 
Balozi  wa Samsung Tanzania,Aisha Saki(kulia) akimuelekeza jambo mteja katika  kipeperushi alipotembelea uzinduzi wa simu ya Samsung Galaxy S7 Mlimani City jijini Dar es Salaam.Kulia ni mabalozi wenzake wakizungumza na wateja.
Balozi wa Samsung Tanzania,RhodaIddy(kulia) akimkabidhi mteja simu ya Samsung Galaxy S7 baada ya kuinunua mara baada ya uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Samsung Tanzania,Neema Mziray (katikati) akiwaelezea jambo wateja kuhusu ubora wa simu ya Samsung Galaxy S7 mara baada ya uzinduzi uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Samsung Tanzania,Neema Mziray (katikati) akiwaelezea jambo wateja kuhusu ubora wa simu ya Samsung Galaxy S7 mara baada ya uzinduzi uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Samsung Tanzania,Neema Mziray (kushoto) akimuonyesha mjeta Gear VR inavyoweza kufanya kazi kwa kutumia simu ya Samsung Galaxy S7 mara baada ya uzinduzi uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Samsung Tanzania,Neema Mziray (kushoto) akimuonyesha mjeta Gear VR inavyoweza kufanyakazi  kwakutumia simu ya Samsung Galaxy S7 mara baada ya uzinduzi uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.


Samsung Tanzania yazindua Simu ya Galaxy S7
KAMPUNI ya Samsung nchini Tanzania imezindua simu mpya ya Samsung Galaxy S7 Mlimani City jijini Dar es Salam.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja mafunzo wa bidhaa za Samsung, Julius Giabe mara baada ya uzinduzi alisema simu ya Samsung Galaxy S7 ni toleo jipya ambalo kwa sasa inapatikana madukani kote nchini.
Amewaomba watanzania wajitokeze kununu simu hiyo yenye ubora wa hali ya juu kwani imeboreshwa zaidi kulingana na tekinolojia ya sasa.
Alisema  Julius Samsung Galaxy S7 imeboreshwa zaidi kwenye upande wa Camera kwani ina Mega Pixel 12 zilizoboreshwa zaidi kiasi ambacho unaweza kupata picha au Video nzuri zaidi.
Kioo chake kizuri cha kuvutia na inazuia vumbi na Maji kwa muda wa dakika 30 ndani y maji.
Julius alisema, Samsung Galaxy S7 inakaa na chaji kwa muda mrefu sana na hata ikiisha chaji inauwezo wa kuichaji bila kuchomeka kwenye Umeme(Wireless charging)
Julius alimaliza kwa kuwaomba watanzania tusikose kumiliki simu ya Samsung Galaxy S7 ukakosa mambo mazuri katika teknolojia hii ya kisasa ambayo Dunia yote iko Kiganjani mwako.
Kwa wakazi wa Dar es Salaam tutembelee Mlimani City ambapo promosheni ya Samsung Galaxy S7 inaendelea,upate kwa undani ubora wa simu hiyo.

“Kuwa wa kwanza kumiliki simu ya Samsung Galaxy S7”.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.