Mbunge wa viti maalum Faharia Khamis Shomari akizungumza na Wajumbe wa Umoja wa WanawakeTanzania (UWT) katika ukumbi wa CCM Mkoa pichani hawapo kwenye sherehe ya makabiziano ya magari hayo yalio fanyika katika Ukumbi wa CCM Mkoa Amani Zanzibar.
Mhe: Faharia Shomari Khamis akimkabidhi funguo Mgeni Rasmi katika sherehe za Makabidhiano Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai kwaajili ya kuwakabidhi wahusika.
Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akitoa shukurani kwa Mhe Faharia na kuwataka wanawake wengine kuiga mfano wake wa kujitolea ndani ya chama,hafla ya Makabidhiano hayo ilifanyika katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akimkabidhi funguo za Gari Mwakilishi wa Umoja wa Wanawake UWT Tanzania Asha Mzee ambazo zimetolewa na Mhe. Faharia Shomari Khamis.
Mwakilishi kutoka Umoja wa Wanawake UWT Tanzania Asha Mzee akilifungua gari walilokabidhiwa na Mhe. Faharia Shomar Khamis.
Magari aina ya Noha waliokabidhiwa Umoja wa Wanawake UWT Tanzania.(Picha na Abdalla Omar – Maelezo Zanzibar.).
No comments:
Post a Comment