Tuesday, June 7, 2016

Mradi wa Kuhuisha Eneo Ngambo Kuwa Kituo cha Mji wa Zanzibar, Ngambo Tuitakayo Maeneo ya Muemberikunda, Muembeladu, Kisimajongoo Vikokotoni

  
Muonekano wa majengo yatakayokuwa katika Mradi wa Ngambo Tuitakayo yatakayojengwa katika maeneo hayo. 

Mandhari inayoonekana pichani ni sehemu ya Michenzani ikigawa maeneo ya Mradi wa Ngambo Tuitakayo itakayojengwa majengo ya kisasa ya mji wa ngambo.
Wanafunzi wa Skuli wakicheza ngoma ya Mwanandege wakati wa uzinduzi wa maonesho ya michoro na picha za mradi wa ngambo tuitakayo itakayojengwa katika maeneo ya ngambo katika maeneo ya muembeladu, muembetanga muemberikunda na kikwajuni Unguja.
Mwakilisho wa Ubalozi wa Uholanzi Mr.Eugen Gies, akipokea Ndege wakati wa Uzinduzi huo wa Maonesho ya Ngambo Tuitakayo yaliofanyika katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani Kisonge Zanzibar.
Wageni waalikwa wakifuatilia ngoma wakati wa uzinduzi huo wa maonesho hayo viwanja vya mnara wa kumbukumbu michezani kisonge zanzibar. 
Wasanii wa Kikundi cha Tausi wakisoma Maulidi ya Homu wakati wa maonesho hayo. 

Muwezeshaji wa hafla hiyo Ndg Mohammed Zahrani akitowa maelezo wakati wa hafla hiyo.

Mkurugenzi Miji na Vijiji Zanzibar Dk. Mohammed Juma, akizungumza Mradi huo wa Ujenzi wa Mji wa Ngambo Tuitakayo yanayotarajiwa kuaza ujenzi wake hivi karibu ili kuuweka mji wa Zanzibar katika hadhi ya kimataifa Zanzibar.