Habari za Punde

Kamati Tendaji ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) lafanya Mkutano wa Maandalizi ya Michezo ya Baraza Hilo Itakayofanyika Zanzibar Mwaka huu.

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) Brigedia Generali Civil Mhaiki akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Muhammed Mahmoud kufungua mkutano wa Kamati Tendaji ya Bara hilo unaofanyika Makao Makuu ya Kikosi cha Valantia Mtoni Mjini Zanzibar, (kulia) Makamu Mwenyekiti wa BAMMATA, CDR wa KMKM Muhammed Ali Bakar.
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Muhammed Mahmoud akifungua Mkutano wa Kamati Tendaji ya BAMMATA wa maandalizi ya michezo ya Baraza hilo unaofanyika Makao Makuu ya Valantia, Mtoni Mjini Zanzibar.
Wajumbe wa Kamati Tendaji ya BAMMATA wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Muhammed Mahmoud (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa maandalizi ya michezo ya majeshi Tanzania itakayofanyika Zanzibar mwaka huu.
Wajumbe wa Kamati Tendaji ya BAMMATA wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Muhammed Mahmoud (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa maandalizi ya michezo ya majeshi Tanzania itakayofanyika Zanzibar mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Muhammed Mahmoud akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya BAMMATA baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Maandalizi ya Michezo ya Majenshi Tanzania itakayofanyika Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.