Habari za Punde

Mbabe wa Wawi Star Avuna Alichopanda.

Na: Abdi Suleiman, PEMBA.


ZFA Taifa Pemba imemfungia michezo mitatu na kumpiga faini ya shilingi Elfu 50,000/= mchezaji wa Wawi Star Salum Abdalla Juma, kwa kosa la kumpiga mchezaji wa timu ya Okapi.

Hatu hiyo imekuja baada ya ZFA kupitia Ripoti ya Kamisaa na Mwamuzi wa Mchezo huo wa Oktoba 25 mwaka huu, uliopigwa katika kiwanja cha Michezo Gombani, huku Wawi Star ikifungwa goli 3-0.

Katibu Msaidizi wa ZFA Taifa Pemba, Khamis Hamadi alisema adhabu hiyo ni kwamujibu wa kanuni ya kuendeshea mpira wa miguu kifungu No.16 (C) faini ambayo inatakiwa kulipwa sizaidi ya Novemba 11 mwaka huu.

“Kwa Makusudi Salum Abdalla alithubutu kumpiga ngumi mchezaji wa timu pinzani na kumsababishia maumivu kitu ambacho hakikubaliki”alisema.

Alisema kitendo kilichofanywa na mchezaji huyo wa Wawi Star, sio kitendo cha Kiungwana na hakikubaliziki kabisa michezoni, huku akiwataka wachezaji kujiepusha na matukio yanayoweza kuigharimu timu yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.