Habari za Punde

Naibu Katibu Mkuu CCM Ziarani Pemba.

Na Salmin J. Salmin Pemba.

 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai fanya ziara ya Kichama Kisiwani Pembe,na kuwataka Wana CCM, katika Jimbo la Kojani kuendeleza umoja na mshikamano uliopo na kujiepusha na migogoro miongoni mwao. Ameyasema hayo akiwa katika ziara yake katika jimbo hilo leo.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Wanachama wa CCM wa Kojani na kuwataka kuzitetea sera za CCM ni umoja na mshikamano ambapo kila mwanachama anapaswa kuzitekeleza ili kuleta umoja katika jamii, na kuimarisha Chama cha Mapinduzi.

Katika ziara yake hiyo amepokea Wanachama Wapya waliojiunga na CCM katika jimbo hilo 80 na kuwakabidhi kadi 

Amesema Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai wananchi wa jimbo hilo hawana budi kujivunia maendeleo yaliofanywa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayongozwa na Dk Shein, katika kuwaletea maendeleo na kutatua matatizo ya Wananchi wa Zanzibar katika kuwaletea maendeleo.

Amewataka Wanawake kujitokeza katika kugombea nafasi za Uongozi katika Ngazi mbalimbali za Chama na Jumuiya zake katika chaguzi zinazotarajiwa kufanyika hivi karibuni wakati ukifika. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.