Ofisi
ya Taifa ya Takwimu
Simu: 255- (022) 2122722/3/4
|
18 Barabara ya Kivukoni,
|
Nukushi: +225 (022)2130852
|
S. L. P 796,
|
Barua pepe: dg@nbs.go.tz
|
11992 Dar es Salaam,
|
Tovuti: www.nbs.go.tz
|
TANZANIA.
|
TANGAZO
Ofisi
ya Taifa ya Takwimu (NBS) inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa yeyote
anayetaka kuwa Mdadisi au Mkusanyaji taarifa za kitakwimu rasmi katika tafiti
mbalimbali zinazoratibiwa na ofisi hii, ni sharti awe amehitimu Mafunzo ya Ukusanyaji
Takwimu Rasmi angalau kwa ngazi ya cheti.
Hii ni kwa mujibu wa Sheria
ya Takwimu Na. 9 ya mwaka 2015 inayoipa mamlaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya kuratibu
na kusimamia ukusanyaji takwimu rasmi (official statistics) nchini.
Hivyo,
kuanzia sasa NBS itakuwa inawatumia wadadisi ambao wamehudhuria na kuhitimu angalau
cheti cha Ukusanyaji Takwimu katika miradi mbalimbali ili kuboresha zaidi
upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.
Mafunzo ya Ukusanyaji
Takwimu Rasmi yanatolewa na Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika “Eastern
Africa Statistical Training Centre” (EASTC) kilichopo Changanyikeni jijini Dar
es Salaam.
Kwa
mawasiliano zaidi na kujisajili wasiliana na:
Ofisi
ya Msajili wa Chuo,
Eastern
Africa Statistical Training Centre,
S.L.P
35103,
DAR
ES SALAAM.
Barua
pepe: info@eastc.ac.tz;
Tovuti:
www.eastc.ac.tz
Simu
namba: 022-2925000 au 0784784106.
Tangazo hili
limetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu,
Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
DAR ES SALAAM.
05 Oktoba, 2016.
No comments:
Post a Comment