Habari za Punde

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Mkoani awataka vijana kutunza amani iliyopo


Kamanda wa polisi wilaya ya Mkoani Mohamed Salim, amewaonya vijana kuwa makini katika kutunza amani iliopo, ili kuepusha kutokea vitendo vibaya visivyokuwa na umuhimu kwa taifa lao. 

Amesema kuvunjika kwa amani kunasababisha kuibuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, kuanguka uchumi sambamba na matendo ya ubakaji, unyanyasaji na wizi kujitokeza. 

Kamanda Mohamed ametowa nasaha hzio skuli ya maendeleo Ngwachani kwenye mdahalo uliowashirikisha vijana wa mabaraza ya vijana ya wilaya ya mkoani ulioandaliwa na jumuiya ya uzalishaji wa karafuu na viungo pemba jukavipe wakati wakijadili mada ya kutunza amani na kutii sheria bila ya kushurutishwa. 

Akivitaja viashiria vya uvunjifu wa amani Kamanda Mohamed amesema ni pamoja na migongano kwa kutokuwepo makubaliano kati ya mtu na mtu au kikundi na kikundi, hali ambayo inaweza kuzalisha vita ambavyo vinaweza kuleta uvunjifu wa amani. 

Akifunga mdahalo huo Mkurugenzi wa jukavipe, Hassan Ali Bakar amesema jumuiya hiyo ilisikitishwa sana kuona mikarafuu iliyoteketezwa mara baada ya uchaguzi katika vijiji mbali mbali. 

Washiriki wa mdahalo huo wamelalamikia usimamizi na utekelezaji wa sheria wakati wa kutoa maamuzi ya matukio mbali mbali kwamba hauwaridhishi wananchi.

Credit. ZBC

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.