Habari za Punde

Mwakilishi wa Unesco atembelea Redio Jamii kisiwani Pemba

 MWAKILISHI wa shirika la kimataifa la UNESCO na Mfuko kwa ajili ya kuwaendeleza wanahabari Tanzania TMF, Kiondo Mshana (mwenye suti), akisalimiana kwa mtindo wa kukumbatiana na Meneja wa Redio Jamii Mkoani Pemba, Ali Abass Omar, wakati mwakilishi huyo alipofika hapo kuzungumza na Meneja huyo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MWAKILISHI wa shirika la kimataifa la UNESCO na Mfuko kwa ajili ya kuwaendeleza wanahabari Tanzania TMF, Kiondo Mshana (kulia), akizungumza na Meneja wa Redio Jamii Mkoani Pemba, Ali Abass Omar, mazungumzo hayo yalifanyika kituoni hapo Mkanyageni Mkoani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MWANDISHI wa habari wa shirika la Magazeti ya serikali kisiwani Pemba, Haji Nassor, akiwafahamisha waandishi na watangaazaji wa Redio Jamii Mkoani, jinsi ya kupata habari za kila siku ndani ya wilaya hiyo, (Picha na Ali Suleiman, Pemba).
 DIWANI wa wadi ya Ngwachani wilaya ya Mkoani Pemba, Salum Omar akimuonyesha Mwakilishi  wa shirika la kimataifa la UNESCO na Mfuko kwa ajili ya kuwaendeleza wanahabari Tanzania TMF, Kiondo Mshana , namna karafuu zainavyozaliwa, eneo la Mgagadu wilaya ya Mkoani, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja kisiwani Pemba, ya kuzitembelea redio jamii za Mkoani na Micheweni, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MENEJA wa redio Jamii Micheweni Kaskazini Pemba, Ali Massoud Kombo (kulia), akiwa na Mwakilishi  wa shirika la kimataifa la UNESCO na Mfuko kwa ajili ya kuwaendeleza wanahabari Tanzania TMF, Kiondo Mshana, wakiingia kwenye kituo cha Redio jamii Micheweni, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja kisiwani humo, ya kuzitembelea redio jamii Mkoani na Micheweni, (Picha na Haji Nassor, Pemba).


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.