Habari za Punde

Maziko ya Mzee Taimour Saleh leo

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) alipojumuika na Waislamu mbali mbali katika kumswalia Marehemu Mzee Taimur Saleh Juma katika Msikiti wa Ijumaa Mchangani Mjini leo,marehemu aliwahi kushika nyazifa mbali mbali katika Serikalia ya Mapinduzi Zanzibar,[Picha na Ikulu.]23/05/2017.

 Baadhi ya Waislamu wakiitikia dua iliyoombwa baada ya Swala ya Maiti ya Marehemu Mzee Taimur Saleh Juma  katika msikiti wa Mchangani Mjini,ambapo Viongozi mbali mbali wa Serikali na Vyama vya Siasa walihudhuria na kwenda kuzikwa katika makaburi ya Kianga alipozikwa Marehemu huyo leo,[Picha na Ikulu.]23/05/2017.
 Viongozi na Waislamu wakilibeba jeneeza la mwili wa Marehemu Mzee Taimur Saleh Juma baada ya kuswaliwa katika Msikiti wa Ijumaa Mchangani Mjini na kuelekea katika mazishi yake yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kianga wilaya ya Magharibi "A"Unguja,[Picha na Ikulu.]23/05/2017.

 Baadhi ya waislamu na Wananchi mbali mbali wakilibeba jeneeza lenye mwili wa Marehemu Mzee Taimur Saleh Juma baada ya kuswaliwa katika Msikiti wa Ijumaa Mchangani Mjini na kuelekea katika mazishi yake yaliyofanyika leo makaburi ya Kianga wilaya ya Magharibi "A"Unguja,[Picha na Ikulu.]23/05/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) alipojumuika na Viongozi mbali mbali na Waislamu  katika kumzika Marehemu Mzee Taimur Saleh Juma katika makaburi ya Kianga Wilaya ya Magharibi "A" Unguja yaliyofanyika leo,[Picha na Ikulu.]23/05/2017.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.