Habari za Punde

Mwembe wasitisha safari dakika 45 Pemba

WANANCHI wa kisiwa cha Makoongwe wilaya ya Mkoani Pemba, wakiwa safarini ndani ya mashua yenye mashine, wakitokea Mkoani mjini kwenda kijijini kwao, ambapo hayo ndio maisha yao ya kila siku
IPO haja kwa wazazi na walezi, kuwa makini na maeneo wanayocheza watoto wao, ambapo mtoto ambae hakupatikana jina lake, akikata tawi, alilolikalia karibu na skuli ya Makoongwe wilaya ya Mkoani
MWANDISHI wa Shirika la Magazeti ya Serikali ofisi ya Pemba Haji Nassor, akizungumza na Mwenyekiti Jumuia ya Sanaa, Elimu ya Ukimwi na Mazingira JSEUMA, Juma Ali Mati juu ya hatua waliofikia, ndani ya jumuia yao, kuhusu kuwaelimisha wananchi kupanda miti na kuhifadhi mazingira, (Picha na Zuhura Msabaha, Pemba).
Mwananchi wa shehia ya Mkanyageni wilaya ya Mkoani Pemba alietambulika kwa jina Seif, akichangia jambo kwenye mkutano wa uhamasishaji wa upandaji miti uliondaliwa na Jumuia ya Sanaa, Elimu ya Ukiwmi na , Mazingira JSEUMA ya Kisiwani panza, wilaya ya Mkoani Pemba. 
Waandishi wa habari kisiwani Pemba, wakisikiliza mada kwenye mmoja ya mikutano iliofanyika hivi karibuni kwenye uwanja wa Gombani Chakechake Pemba, ambao uliandaliwa na kitengo cha malaria Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

Na. Haji Nassor. Pemba.

ABIRIA waliokuwa wakitokea Unguja, wafanyakazi wa serikali na taasisi binafsi pamoja na wananchi wengine, juzi walilazimika kusubiri kwa dakika 45, kwenye eneo la mpakani baina ya wilaya za Mkoani na Chakechake, kufuatia mti aina ya Muwembe kukatika na kuziba barabara.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, abiria na wananchi hao walisema, baada ya kuteremka meli bandari ya Mkoani, walipanda gari za abiria ili kuelekea kwenye mkaazi yao, ingawa walipofika mpakani walikwama.

Walisema walikaa hapo tokea majira ya saa 10:30 hadi saa 11:15 ndipo walipofanikiwa kupita baada ya taasisi kadhaa wakiwemo idara ya misitu kukakata Muwembe.

Walisema kama sio taasisi za serikali zikiwemo KZU, Idara ya misitu na wananchi wanaoishi karibu na eneo hilo la Vuleni kushirikiana wengeutumia hadi saa 1:30.

Mmoja kati ya abiria aliekuwa akitokea Unguja, Juma Mshihiri Hassan mkaazi wa Konde, alisema baada ya kufika hapo walishuhudia foleni ya gari zaidi ya 30 na waliarifiwa kwamba barabara imefungika, kutokana na kuanguka Muwembe katikati.

Nae Asha Msabaha Himid wa Chasasa alisema, alitarajia akapeleke mzigo kwao, kisha arudi bandarini kwa vile siku ya pili alikuwa anasafiri, ingawa kutokana na kuchelewa kuondoka hapo itakuwa vigumu.

“Sisi tupo hapa zaidi ya dakika 45, maana tunakaribia tu na Muwembe huo unanguka, na kuziba njia yote, maana upande mwengine kuna bonde, hapana pakukimbilia, ingawa baadae walikuja watu kuukata na kuondoka’’,alisema.

Hata hivyo dereva wa gari ya Chakechake –Mkoani aliejitambulisha kwa jina moja la ‘Kipara’ alisema katika kipindi hichi cha mvua, lazima wawe makini maana miti huunguka kutokana na ardhi kushiba maji.

Kwa upande wake dereva aliefanikiwa kupenya kwenye eneo hilo la Vuleni na kisha Muwembe kuanguka,  Ali Haji Juma, alisema aliouna umeshainama, ingawa baada ya nusu saa aliamua kupita salama.

“Mimi baada ya kupita dakika 10 tu, napata taarifa kuwa, umeshanguka na gari zimekwama, ingawa na juzi nilikwama Ngwachani baada ya Muwembe kuanguka na kuziba arabara’’,alifafanua.

Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Mkoani ambae nae juzi ni miongoni mwa wananchi waliokwama,  Hemed Suleiman Abdalla, aliwashukuru watendaji wa taasisi mbali mbali, kwa umoja na mshikamano wao.


Tokea kuanza kwa mvua hizi za masika, tayari miti zaidi ya sita imeshaanguka na kuziba barabara ikiwemo eneo la Ngwachani, Ngezi, Vuleni na Mtambile.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.