Habari za Punde

Umaskini Watajwa Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu.

Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu, ambae pia ni Mgeni Rasmi, Adatus Magere akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya kuzuia biashara hiyo. Kulia ni Mratibu wa Mradi wa Shirika la Wahamiaji la Kimataifa, Tamara Keating. Mafunzo hayo yanashirikisha wadau mbali mbali kutoka katika nchi zilizopo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).Mafunzo hayo yanafanyika jijini Dar es Salaam
Afisa Mkuu wa Kitengo cha Jinsia kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Dk. Joseph Pitso, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu. Wengine ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya kupambana na biashara hiyo, ambaye pia ni Mgeni Rasmi, Adatus Magere na Mratibu wa Mradi wa Shirika la Wahamiaji la Kimataifa nchini, Tamara Keating. Mafunzo hayo yanashirikisha wadau mbali mbali kutoka katika nchi zilizopo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).Mafunzo hayo yanafanyika jijini Dar es Salaam
Mratibu wa Mradi wa Shirika la Wahamiaji la Kimataifa nchini, Tamara Keating, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu,Wengine ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu, ambae pia ni Mgeni Rasmi, Adatus Magere na Afisa Mkuu wa Kitengo cha Jinsia kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Dk. Joseph Pitso. Mafunzo yanashirikisha wajumbe kutoka katika nchi zilizomo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)  hayo yanafanyika jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu, ambae pia ni Mgeni Rasmi, Adatus Magere akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya kuzuia biashara hiyo. Kulia ni Mratibu wa Mradi wa Shirika la Wahamiaji la Kimataifa, Tamara Keating. Mafunzo hayo yanashirikisha wadau mbali mbali kutoka katika nchi zilizopo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).Mafunzo hayo yanafanyika jijini Dar es Salaam

Mratibu wa Mradi wa Shirika la Wahamiaji la Kimataifa nchini, Tamara Keating, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu,Wengine ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu,ambae pia ni Mgeni Rasmi, Adatus Magere na Afisa Mkuu wa Kitengo cha Jinsia kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Dk. Joseph Pitso. Mafunzo yanashirikisha wajumbe kutoka katika nchi zilizomo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)  hayo yanafanyika jijini Dar es Salaam. 
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Na Mwandishi Wetu.

Hali ngumu ya maisha ikiwepo ukosefu wa mahitaji muhimu imetajwa kama sababu kubwa inayochochea Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu huku waaathirika wa biashara hiyo wakiahidiwa maisha mazuri katika nchi wanazopelekwa.

Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu (ATP), ambaye pia ni mgeni rasmi katika mafunzo hayo, Adatus Magere amesema wahusika wa biashara hiyo wamekuwa wakiwarubuni waathirika wa biashara hiyo kuwapatia maisha mazuri na kujikuta wakiingia katika madhara ya biashara hiyo.

Aliongeza kuwa kuna umuhimu kwa watunga sheria na vyombo vya sheria kutunga sheria zitakazosaidia kutokomeza kabisa biashara hiyo kwani imekua ikiendelea kukua siku hadi siku hali inayopelekea idadi ya wahanga wa biashara hiyo kuendelea kuongezeka.

“Tunaomba watunga sheria na wasimamiaji wa sheria kusaidiana kwa pamoja katika kudhibiti na kuzuia biashara hiyo kwa kutoa adhabu kali kwa wale watakaobainika kuhusika moja kwa moja na biashara hiyo ili tatizo hili liweze kuisha katika nchi zetu,” alisema Magere.

Aidha Katibu Mkuu wa Sekritarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu ambaye pia ni mwenyeji kwenye mafunzo hayo, Seperatusi Fella, amesema kuwa ili kuweza kupambana na kuzuia biashara hiyo kuna umuhimu kwa wadau mbali mbali kutoa elimu na mafunzo juu ya athari zitokanazo na usafirishaji haramu wa binadamu, hivyo mafunzo ya mara kwa mara ni muhimu kwa wananchi na wadau mbali mbali.

Naye Mratibu wa mradi wa Shirika la Wahamiaji la Kimataifa (IOM), Tamara Keating ameahidi kushirikiana na mashirika mbali mbali ili kukomesha biashara hiyo sambamba na kutoa elimu kwa wananchi ili kupata taarifa ya wahusika wa biashara hiyo.

Ripoti na tafiti mbali mbali za kimataifa juu ya biashara hiyo zinaonesha Tanzania ni moja wapo kati ya nchi nyingi zinazohuishwa na biashara haramu ya usafirishaji binaadamu ambapo waathirika wengi wa biashara hii ni watoto waliochini ya umri wa miaka 18 na kuendelea wanaoahidiwa kazi nzuri na maisha mazuri pindi wafikapo katika nchi wanazopelekwa.

Mafunzo hayo yanafanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam yakiwa na lengo la kuleta uelewa wa jinsi biashara hiyo inavyoendeshwa pamoja na kuleta ushirikiano katika kukomesha biashara haramu ya usafirishaji binadamu baina ya wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.