STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Pemba
23.08.2017
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, amesema kuwa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa huduma zote muhimu kwa wananchi wake
zikiwemo huduma za afya bila ya ubaguzi.
Dk. Shein aliyasema hayo leo, huko Junguni, Wilaya
ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba mara baada ya kuzindua Kituo cha Afya cha Mama
na Mtoto, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake kiswani Pemba.
Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa kamwe
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitombagua mtu yoyote kwa itikadi yake ya
kisiasa na badala yake itahakikisha wananchi wote Zanzibar wanapata huduma muhimu
za maendeleo.
Dk. Shein alisema kuwa mwananchi yeyote anaekwenda
kituoni hapo kupata huduma za afya hatabaguliwa kwani yeye ni mwananchi wa
Zanzibar na akiwa mzazi atazalishwa kwa kufuata taratibu zote kwa mujibu wa
taaluma aliyosomeshwa na Serikali.
Aidha, Dk. Shein alieleza kuwa iwapo mwananchi
atajibagua mwenyewe kwa kutokwenda kituoni hapo kupata huduma hiyo itakuwa si
lawama kwa Serikali kwani juhudi kubwa zimekuwa zikichukuliwa na Stikali ili
wnannchi wote wapate huduma muhimu bila ya ubaguzi.
Aliongeza kuwa chama chochote duniani
kinachoongoza nchi kikipeleka maendeleo basi hakiwakusidi wanachama wake pekee
bali huwakusudia wananchi wote.
Pamoja na hayo Dk. Shein alilihakikishia Shirika
la Umoja wa Mataifa linalohudumia idadi ya Watu Duniani (UNFPA) kuwa Serikali
ya Mainduzi ya Zanzibar inatambua wajibu wake na imo katika kutekeleza wajibu
huo ambao umeelekezwa tokea wakati wa ASP mbapo katika Ilani yake ilielekeza
hivyo.
Alisema kuwa Setikali haiwezei kuepuka wajibu wake
katika kuwapelekea huduma muhimu wananchi wake lakini kinachokwamisha ni uhaba
wa nyenzo na fedha lakini hata hivyo juhudi za makusudi huchukuliwa ili
kuhakikisha mafanikiio yanapatikana.
Pia, Dk. Shein aliwataka akina baba kuwapa moyo
wake zao wakati wanapokuwa wajawazito hata pale wanapojifungua kuwa nao karibu
huku akieleza azma ya Serikali katika kuhakikisha vifo vya akina mama wajazito
vinapungua kwa kiasi kikubwa.
Dk. Shein aliwahakikishia wananchi kuwa huduma za
afya zitaendelea kuwa bure hasa kwa akina mama wajawazito ila pale panopotokea
upungufu wa vifaa kuna haja ya kuchangia huku akitoa maagizo ya kupelekwa
ultrasound pamoja na wafanyakazi ili kuondoa changamoto ya wafanyakazi kituoni
hapo.
Sambamba na hayo, Dk. Sgein alitumia fursa hiyo
kutoa pongezi kwa Shirika la UNFPA kwa kuendelea kuisaidia Zanzibar kwani
juhudi hizo zimeanzwa kuchukuliwa kipindi kirefu na Shirika hilo na Serikali
itaendelea kufanya kazi pamoja na kushirikiana nalo.
Nae Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman
alieleza kuwa katika kutoa huduma za afya hakuna haja ya ubaguzi na wafanyakazi
wote wa Wizara hiyo wakiwemo wafanyakazi wa kituo hicho wamekuwa wakitoa huduma
zao bila ya ubaguzi kama.
Naibu Waziri huyo alieleza kuwa wananchi wa
Njuguni wamekuwa wakitoa mashirikiano makubwa kwa kutambua kuwa maendeleo
hayana ubaguzi.
Mapema Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Asha Abdalla
alieleza kuwa ujenzi wa kituo hicho cha afya umefanyika chini ya Mradi wa Afya
bora unaofadhiliwa na Serikali ya Canada kupitia Shirika la kuhudumia watoto
UNICEF na Shirika la Idadi ya watu Duniani UNFPA.
Alisema kuwa lengo kuu la mradi huo ni kuimarisha
afya ya mama na motto kupitia uimarishaji wa miundombinu ya afya na uzazi na
kuhakikisha upatikanaji wa huduma za dharura wakati na baada ya kujifungua.
Aliongeza kuwa jumla ya vituo sita katika ujenzi
huo unaojumuisha utanuzi wa wodi za uzazi katika vituo hiyo na kusaidia
upatikanaji wa vifaa muhimu katika utoaji wa huduma za uzazi ambapovituo
viliomo katika mradi huo ni Junguni, Bogoa na Uondwe kwa Pemba na Fuoni, Sebleni
na Tumbatu kwa Unguja.
Aidha, alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho cha afya
cha mama na motto umegharimu kiasi cha TZS milioni 165.8 pamoja na vifaa vyenye
thamani ya TZS 107 ambapo kituo hicho kinahudumia watu 5,074 wa vijiji 16.
Nae Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linalohudumia Idadi ya Watu Duniani UNFPA nchini Tanzania Dk. Hashina Begum
alisema kuwa lengo kubwa la misaada inayotolewa na Shirika hilo ni kuimaisha
mifumo ya afya iliiweze kutoa kwa usawa huduma jumuishi za kiafya.
Pamoja na kuimaisha huduma za rufaa na kuongeza
ubora katika kufikia na kutoa huduma za dharura za uzazi kwa mama, huduma za
watoto wachanga pamoja na huduma za afya kwa wavulana na wasichana.
Alieleza kuwa lengo kubwa la Mradi huo ambao
unajulikana pia kama ‘ Afya Bora ya Mama na Mtoto’ ni kuimarisha afya na ustawi
wa mama, wavulana, wasichana na watoto hapa Zanzibar huku akiahidi kuwa Shirika
hilo litaendelea kuiunga mkono Zanzibar.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment