STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 24.9.2017

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa
mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na kumuapisha Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utumishi wa
Umma pamoja na Wajumbe wake.
Viongozi walioapishwa
na Rais Dk. Shein katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar hivi leo ni Dk.
Idris Muslim Hija ameapishwa kuwa Katibu Mkuu
wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Joseph Abdulla Meza ameapishwa kuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Juma Ali Juma ameapishwa
kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko.
Bakari Haji Bakari ameapishwa kuwa Katibu Mtendaji
wa Baraza la Biashara la Zanzibar, Bwana Ali Khamis Juma ameapishwa kuwa Naibu
Katibu Mkuu katika Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko, Iddi Haji Makame ameapishwa
kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Fedha na Mipango.
Wengine ni Abeid Juma Ali ameapishwa kuwa Mkuu wa
Wilaya ya Wete – Pemba, Rashid Hadid Rashid ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Chakechake- Pemba, Salama Mbarouk Khatib ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni-Pemba
na Kapteni Khatib Khamis Mwadini ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A,
Unguja.
Wakati huo
huo, Rais
Dk. Shein amemuapisha Mohammed Fakih Mohammed kuwa
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma,
pamoja na kuwaapisha Wajumbe wa Kamisheni hiyo akiwemo Balozi Hussein Said
Khatib, Jaji Hamid Mahmoud Hamid, Mabrouk Jabu Makame, Ali Rajab Juma, Issa
Mohamed Suleiman na Rukia Mohamed Issa.
Hafla hiyo, ilihudhuriwa
na viongozi mbali mbali wa Serikali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif
Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi
Zubeir Ali Maulid, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, Mawaziri,
Manaibu Mawaziri, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk.
Abdulhamid Yahya Mzee, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Naibu
Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali.
Na wengine waliohudhuria
hafla hiyo ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi
Ayoub Mohamed Mahmoud, Washauri wa Rais wa Zanzibar, Meya wa Manispaa ya Mji wa
Zanzibar Khatib Abrahman Khatib pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment