
Akizungumzia
kampeni hiyo Afisa Habari wa Rise Media Bakari Ngamba amesema kuwa kampeni hiyo
imebebwa na kauli mbiu isemayo mtoto kwanza Elimu ni msingi.
“kampeni
hii inamakusudio makuu mawili, moja ikiwa ni kuwasaidia watoto wa shule za
Msingi waishio vijijini vifaa mbalimbali vya kujifunzia ,Pili ni kuhamasisha
watoto kupenda shule na kuwafundisha baadhi ya masomo ya jamii ili waweze kutimiza
ndoto zao, Kampeni hii inatarajiwa kuzunguka mikoa mbalimbali Tanzania ” alisema Ngamba.
Aidha
Ngamba amewakaribisha wadau Mbalimbali wa elimu nchini na nje ya nchi kuungana na
Rise Media kwa kuchangia kampeni hii ili kuendeleza elimu nchini pamoja na
kudumisha elimu kwa wanafunzi katika kuendeleza na kujenga Tanzania ya viwanda kwa kumfunza Mtoto kuwa
na uzalendo wa kujenga nchi yake kwa kusaidia wengine pindi atakavyo kuwa
mkubwa kwani hii ni moja ya kumbu kumbu katika maisha yake.
Vile
vile Rise charity ina dhumuni la kuhamasisha mahusiano mazuri baina ya wazazi na
wanafunzi pamoja na wadau mbalimbali katika kuhakikisha kuwa mtoto anapata
mahitaji muhimu ya kitaaluma kwa wakati uliokusudiwa.
Akieleza
Namna unavyoweza kushiriki katika kuchangia kampeni hiyo ni kwa kuwasiliana na Mwenyekiti wa kampeni Ndugu Elia Joseph kwa namba 0716
23 69 12 na Atley Timothy 0719 92 15 64

No comments:
Post a Comment