Mwenyekiti wa Bodi ya
Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Bw. HAB Mkwizu (kulia) akizungumza na
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza
(katikati) alipofanya ziara katika Kampuni hiyo jana Jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji TSN Dkt. Jim Yonazi
Mkurugenzi Mtendaji TSN Dkt. Jim Yonazi
akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) katika Kampuni hiyo jana Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Wizara
ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akizungumza
na Menejimenti ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) alipofanya ziara katika
Kampuni hiyo jana Jijini Dar es Salaam
Mhariri wa gazeti la
Daily News Bw. Leonard Mwakalebela (kushoto) akimwelezea Naibu Waziri Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) namna habari
zinavopitiwa na kupangwa katika gazeti hilo alipofanya ziara katika kampuni ya
TSN jana Jijini Dar es Salaam
Meneja wa uchapishaji
wa magazeti ya Serikali Bw. Boniface Mwajombe (kulia) akimuonyesha Naibu Waziri
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati)
mpangilia wa habari unavokuwa kabla ya gazeti kuchapishwa wakati wa ziara ya
Naibu Waziri huyo katika kampuni ya TSN jana Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Wizara
ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akiangalia mashine ya
kuchapishia magazeti ya Serikali inavyofanya kazi alipofanya ziara katika
Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) jana Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Wizara
ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (watano kushoto)
katika picha ya pamoja na menejimenti ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN)
alipofanya ziara katika kampuni hiyo na kuangali shughuli zinazofanywa na
kampuni hiyo jana Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayob Rioba (kushoto)
akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Juliana Shonza (kulia) alipofanya ziara TBC jana Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Wizara
ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati)
akimsikiliza Mkuu wa TBC Fm Bw. Othuman Iddy (kushoto) alipotembelea studio za
TBC Fm wakati wa ziara yake TBC jana Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Wizara
ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati)
akimsikiliza mkuu wa TBC International Bw. Deogratius Salufu (kulia)
alipotembela studio za redio hiyo jana wakati wa ziara yake katika Shirika la
Utangazani la Taifa (TBC) Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Wizara
ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) akiwa katika
meza ya kusomea taarifa ya habari ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) jana
wakati wa ziara yake katika TBC Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi
Mkuu Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayob Rioba
Naibu Waziri Wizara
ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (watatu kushoto)
katika picha ya pamoja na menejimenti ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC)
jana wakati wa ziara yake TBC Jijini Dar es Salaam.
Watatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu TBC Dkt. Ayob Rioba
Picha
na:
Genofeva Matemu - WHUSM
Na: Genofeva Matemu –WHUSM
Naibu Waziri Wizara
ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amevitaka vyombo vya
habari vya serikali kufuata maadali na miiko ya uandishi wa habari kwa
kuzingatia weledi ili umma eweze kupata habari zilizokidhi vigezo vya uandishi
wa habari.
Rai hiyo ameitoa jana
jijini Dar es Salaam alipofanya ziara katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali
(TSN) pamoja na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na kuzungumza na watendaji
wa taasisi hizo.
“Vyombo vya habari
vya serikali viwe mfano bora kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa
watanzania wanapata taarifa sahihi na kwa wakati kwani vyombo hivi ni moja kati
ya mhimili mkubwa wa nchi na kama vitatumika vibaya madhara yake ni makubwa
sana” amesema Mhe. Shonza
Aidha Mhe. Shonza
amesema kuwa Serikali inathamini na kutambua mchango unaotolewa na vyombo vya
habari vikiwemo vyombo vya serikali TBC katika kufikisha taarifa za ukweli na
uhakika katika jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mkuu Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayob Rioba amemhakikishia Mhe.
Shonza kuwa TBC itaendelea kuzingatia weledi na maadili katika kuhabarisha umma
huku ikiendelea kubuni vipindi mbalimbali vitakavovutia jamii kuangalia
televisheni hiyo.
Naye Mkurugenzi
Mtendaji Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa TSN
imeendelea kuhakikisha kuwa taifa linahabarishwa kwa hakika kwa kutumia nyenzo
mbalimbali na uzoefu tangu ilipoanzishwa miaka 88 iliyopita hivyo kuchangia katika
maendeleo ya nchi yetu
“kwa sasa TSN ni
zaidi ya magazeti, imejikita zaidi kuwa kampuni inayotoa huduma za habari kwa
kutumia nyenzo mbalimbali za kiteknolojia ili kuweza kuendana na kasi ya
maendeleo ya sayansi na taknolojia” amesema Dkt. Yonazi.
No comments:
Post a Comment