Habari za Punde

Benki ya Kilimo Yatinga Hong Kong Kutafuta Fursa za Uwekezaji.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania Bwana Francis Assenga nara baada ya kupitia Mchoro wa Ramani ya Mkakati wa Kiuchumi wa 'One Belt One Road' mjini Hong Kong hivi karibuni kwenye tathmini ya fursa za kiuchumi ambazo Tanzania inaweza kunufaika nazo kupitia Mkakati huo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzainia (TADB) Bwana Francis  Assenga (Katikati) akiwa na viongozi mbali mbali mara baada ya kumalizika kwa Kikao chake na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa China Capital Fund Management (Hong Kong) Bwana James Wang (kushoto kwake). Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa First Shanghai Capital Ltd Bwana Allen Wang; Mkurugenzi wa Landmark Investments Hong Kong na Mjumbe wa Kudumu wa Kamati ya Bunge la China Dr. Annie Wu Chung; Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kuhamasisha Ushirikiano kati ya China na Tanzania Bwana  Joseph Kahama; na Mkurugenzi Mtendaji wa First Shanghai Capital Ltd  Bi. Fanny Lee.





Wawakilishi wa Tanzania Bwana Francis  Assenga (Kaimu Mkuruvenzi Mtendaji wa TADB)  wa pili toka kushoto na Bwana Joseph Kahama (Katibu Mkuu wa Taasisi ya China-Tanzania Friendship Association) wakikabidhiwa Zawadi ya Utambuzi wa mchango wao kwenye shughuli za kiuchumi, kilimo na huduma za jamii kwenye Maadhimisho ya Miaka 35 ya Shule ya Sekondari ya Jiji Hong Kong. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo Bwana Au Kwong Wing na Kukia kabisa ni Mratibu wa Maadhimisho hayo (Mwene shati jeupe).


Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania hivi karibuni ilipiga hodi mjini Hong Kong kujadiliana na Taasisi mbali mbali za Hong Kong na China kuhusiana na fursa za upatikanaji wa fedha kwa ajili ya mitaji na uwekezaji kwenye Sekta ya Kilimo nchini Tanzania.

Katika ziara hiyo iliyoratibiwa na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki na Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kuhamasisha Ushirikiano kati ya China na Tanzania Bwana Joseph Kahama, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bwana Francis  Assenga walikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa makampuni na taasisi kadhaa zikiwamo  Benki ya China; China Capital Fund Management (Hong Kong);  First Shanghai Capital Ltd; Mwakilishi wa China Africa Industrial Forum Ndugu Wenbao Tan ambaye ni Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha China.

Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Japan International Cooperation Foundation Bwana Takashi Kawasaki na Mkurugenzi wa China Biodiversity Conservation and Green Development Foundation Prof. Frederick Charles Dubee.

Miongoni mwa yaliyojiri katika mazungumzo hayo ni jinsi Tanzania inavyoweza kunufaika na fursa zilizopo kwenye Mikakati ya 'Silk Road Economic Belt and the 21st-century Maritime Silk Road', ujulikanao kama 'One Belt and One Road Initiative' (OBOR) ambapo kwa mujibu wa Mkakati huo, Tanzania ndio lango kuu la kuingilia Afrika kwa fursa hizo za kiuchumi na kibiashara toka Asia ambapo Tanzania inakuwa kama kiungo muhimu hivyo kuweza kunufaika zaidi ya nchi nyingine.

Miongoni mwa fursa hizo ni pamoja na kukuza uwekezaji kwenye miundombinu ya aina zote, viwanda vikubwa na vya kati, biashara kati ya Afrika na Asia, na Huduma mbalimbali.

Aidha, Bwana Assenga alikutana pia na akina mama wa shirika lisilo la kiserikali la kukuza uchumi kwa akina mama wa Hong Kong wanamiliki pia Shule ya Sekondari kama mchango wao kwenye huduma za jamii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.