Habari za Punde

Sare na Timu ya Libya Yamsononesha Nahodha wa Timu ya Kilimanjaro Stars Erasto Michuano ya Kombe la Chalenji Nchini Kenya.

Na Abubakar Khatib Kisandu, Machakos Kenya.

Nahodha wa Timu ya 
Taifa ya Tanzania Bara         
(Kilimanjaro Stars) 
Erasto Edward Nyoni 
anaonekana 
kusononeshwa na 
sare waliyotoka na 
Libya baada ya kusema kuwa walitegemea kushinda lakini haikuwa bahati kwao.
Katika mchezo huo wa jana, wa kombe la CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP uliopigwa katika uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos nchini Kenya, Kilimanjaro walipata kazi ngumu mbele ya Waarabu wa Libya na kulazimika mchezo huo kutoka sare ya 0-0.

“Tulitegemea kupata ushindi lakini imeshindikana, Libya ni 

wazuri lakini tunashkuru Mungu kupata alau hiyo point 

moja”. Alisema Nyoni.

Mchezo wa pili Kilimanjaro Stars itacheza na ndugu zao Zanzibar Heroes siku ya Alhamis ya Disemba 7 saa 8:00 za mchana katika uwanja wa Kenyatta .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.