Baadhi ya Wauguzi wa Zanzibar wakishiriki katika maandamano maalumu ya kuadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani Kitaifa imeadhimishwa Zanzibar katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar, wakielekea katika ukumbi huo.wakipita katika barabara ya mnazi mmoja.
Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Bi. Amina Abdulkadir Ali akizungumza na wakunga na Wauguzi katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani iliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar, kushoto Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed.
Mwakilishi kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulika Idadi ya watu (UNFPA)Bi.Batula Abdi Hassan akizungumza na wauguzi walioshiriki maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani katika Ukumbi wa Baraza la Wawawkilishi la zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akimkabidhi cheti mmoja wa Wauguzi bora Bi. Rose Abdalla ambae ni mkufunzi mwandamizi kutoka Chuo cha Taaluma ya Sayansi za Afya ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar
Waziri wa Afya Zanzibar.Mhe. Hamad Rashid Mohamed akiwahutubia Wauguzi na Wakunga Zanzibar wakati wa Siku ya Maadhimisho ya Wakuga Duniani ilioadhimishwa katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar na kuhudhuriwa na Wauguzi na Wakunga wa Hospitali za Zanzibar.
Wauguzi kutoka vituo mbali mbali vya Afya Zanzibar walioshiriki maadhimisho ya siku ya Wauguzi duniani wakimsikiliza Waziri wa Afya (hayupo pichani) katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni (Picha na Abdallah Omar - Maelezo Zanzibar)
No comments:
Post a Comment