Habari za Punde

NHIF Tanga Yahamasisha Wafanyabiashara Kujiunga na Mpango wa Bima ya afya


Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Sophia Kaku kushoto akitoa elimu kwa mkazi wa barabara 20 Jijini Tanga aliyetembea Banda lao lililopo kwenye maonyesho ya kimataifa ya Biashara
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Sophia Kaku kushoto akimmkabidhi vipeperusi Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga,Lupakisyo Kapange  mara baada ya kutembelea Banda leo
 Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Sophia Kaku akisalimiana na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Mwahako alipokwenda kufungua maonyesho hayo
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiteta jambo watumishi wa NHIF Tanga  kushoto ni Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga Sophia Kaku  kulia ni Afisa matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga  Macrina Clemens
 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akisalimiana na Afisa matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Macrina Clemens mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
Huduma za kupima zikiendelea kwenye banda la NHIF
 
 Sehemu ya wananchi Jijini Tanga wakiingia kwenye banda la NHIF kupata huduma za upimaji wa afya zao na namna ya kujiunga na mfuko huo


 Afisa Mdhibiti Viwango na Ubora Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Dkt Lawi Kupaza kushoto akimpima presha mkazi wa Jiji la Tanga wakati alipotembelea banda lao
 
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) umesema watatumia maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea Jijini Tanga kuwahamasisha wafanyabiashara kujiunga nao ili waweze kunifaika na huduma za matibabu pindi wanakuwa wakikumbana na magonjwa mbalimbali.

Hayo yalisemwa jana na Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Sophia Kaku wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao kwenye ufunguzi wa maonyesho ya sita ya biashara ya kimataifa yanayofanyika eneo la Mwahako mjini hapa.

Alisema watakapojiunga nao wataweza kuwa na uhakika wa matibabu wakati wanapougua lakini pia itawawezesha kuepukana na kutumia fedha nyingi pindi wanapokuwa wakiugua zinazotokana na kupanda kwa gharama.

“Ndugu zangu maradhi yanakuja bila taarifa hivyo iwapo tutawekeza kujiunga na mpango wa Mfuko huu unaweza kufaidika na matibabu lakini pia utaepukana na gharama kubwa za matibabu utakazopaswa kulipia wakati unapokumbana na magonjwa mbalimbali “Alisema.

Hata hivyo Sophia alisema pia wanatumia nafasi hiyo kuendelea kuhamasisha wazazi na walezi kuwapa watoto wao uhakika wa matibabu wanapokuwa wakiugua kwa kuingiza kwenye mpango wa Toto Afya kadi ambao utamuwezesha kupata huduma.

“Ndugu zangu lazima tuona namna bora ya kuwapa zawadi nzuri ya matibabu kwenye msimu huu kwa kuwaingiza kwenye mpango wa Toto Afya Kadi kwani hii itawawezesha kupata uhakika wa matibabu pindi wanapoumwa”Alisema.

Maonyesho hayo ambayo yalifunguliwa jana na Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage yamebeba kauli mbiu isemayo Biashara ndio ufunguo wa Tanzania ya Viwanda (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.