Habari za Punde

SERIKALI INATENGA KILA MWEZI MILIONI 55 KWENYE JIJI LA TANGA KUHAKIKISHA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI WANAPATA ELIMU BORA-WAZIRI UMMY




 WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa halfa ya ufunguzi huo wa madarasa na makabidhiano kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga
 Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapha Selebosi akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kushoto  ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salimu
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza kwenye halfa hiyo kushoto  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bombo Denis Mushi akizungumza wakati wa halfa hiyo
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizindua madarasa ya shule ya Msingi Bombo Jijini Tanga kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizindua madarasa ya shule ya Msingi Bombo Jijini Tanga kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akifungua mlango mara baada ya kuzindua  madarasa ya shule ya Msingi Bombo Jijini Tanga kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akingia ndani ya madarasa mara baada ya kuyazindua kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi
 Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kulia akimuonyesha kitu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kabla ya kuzindua madarasa ya shule ya Msingi Bombo Jijini Tanga kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kulia akifurahia jambo na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapa Selebosi mara baada ya kuzindua madarasa ya shule ya msingi Bombo
 Sehemu ya wananchi na viongozi waliohudhuria uzinduzi huo wakifuatilia matukio mbalimbali


 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha akiwa amekalia madawati mara baada ya kufanya uzinduzi huo

Kundi la Wasanii la Tanga Kwanza likitumbuiza kwenye uzinduzi huo
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua madarasa hayo kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi kulia mwenye suti ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimukatika akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Msingi Bombo

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii wanaounda kundi la Tanga Kwanza


WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu amesema serikali kila mwezi imekuwa ikitenga fedha kiasi cha sh.milioni 55 kwenye Jiji la Tanga kwa ajili ya shule za msingi  ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila kuwepo kwa vikwazo na hivyo kupata elimu bora.

Aliyasema hayo wakati ufunguzi na kukabidhi vyumba vya madarasa 11 kwenye shule ya Msingi Bombo kwa halmashauri ya Jiji hilo ambavyo ujenzi wake ulichukua zaidi ya mwaka mmoja na kulazimika wanafunzi kuwepo nje ya madarasa yaliyogharimu kiasi cha zaidi ya Milioni 279 zilizotokana na mapato ya ndani.

Ndani ya kipindi hicho wanafunzi hao walilazimika kuhamia kwenye shule ya Msingi Mkwakwani jambo ambalo lilisababisha msongamano mkubwa ambao uliathiri kwa kiasi kikubwa taaluma.

Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga alisema licha ya hivyo lakini pia serikali imekuwa ikitenga fedha kiasi cha sh.milioni 108 kwa ajili ya shule za Sekondari kwenye Jiji hilo ili kuhakikisha wanaweza kukabiliana na changamoto ambazo zinawakabili kupitia sekta hiyo.

“Ndugu zangu ninafuraha sana leo baada ya kufungua madarasa haya ambayo yamejengwa kwa kiwango kizuri na yatawawezesha wanafunzi kusoma bila kuwepo kwa vikwazo lakini pia kupitia sera ya Rais elimu bure serikali inaleta milioni 55 kila mwezi kusaidia elimu kwa watoto wetu kwenye shule za msingi pia nahaidi kushirikiana nanyi”Alisema.

“Lakini pia kadri tunavyoacha kwenda Marekani na Ulaya ndivyo fedha hizo zinasaidia kutumika kwenye harakati za kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu kwa kuwapa watoto wetu elimu bora “Alisema.

Awali akizungumza katika ufunguzi huo,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga alisema ujenzi wa majengo hayo yaliyotumia zaidi ya milooni 279 zilitokana na mapato ya ndani ya halmashauri na kuongezewa na serikali.

Alisema kutokana na kuwepo kwa hali hiyo wana mpongeza Rais Dkt John Magufuli kupitia Wizara ya Elimu kuweka msukumo wao ambapo alihaidia kuzungumza na Waziri wa Wizara hiyo kuweka mradi wa matokeo kwanza ndio wakapata na kupokea kiasi cha milioni 136.6.

“Katika suala hili naomba nikupongeze sana Mh Waziri Ummy kwa kulipigania Jiji la Tanga ndani na nje kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo hivyo nisema tutaendelea kushirikiana”Alisema.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bombo Denis Mushi aliishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli kwa kuhakikisha ujenzi wa madarasa hayo unakamilika kwa wakati ili wananfunzi waweze kuendelea na masomo.

“Tunaishukuru Serikali kwa kusaidia ujenzi huu lakini Mh Waziri Ummy kwa msukumo mkubwa uliouweka kwenye jambo hilo kwani shule waliokuwa wamehamia ya Mkwakwani walikuwa na msongamano mkubwa na kusababisha kutokupata matokeo mazuri “Alisema (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha )

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.