




sehemu ya vitu ambavyo vilikabidhiw
Wafanyakazi
wa Bandari ya Tanga wametoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani y
ash.milioni 1.5kwa kituo cha wazee wasiojiweza kilichopo eneo la
Mwanzange Jijini Tanga
Msaada wa vitu hivyo ni vyakula mbalimbali ambavyo vitatumika kwa
ajili ya kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitri ambapo halfa ya
makabidhiano ilifanyika juzi kwenye kambi hiyo.
Akizungumza mara
baada ya kukabidhi msaada huo,Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi
Bandari ya Tanga Hassan Senkole alisema waliona ni busara kupunguza
sehemu ya mapato yao katika mwezi mtukufu wa ramadhani kuwasaidia wazee
hao.
Alisema waliamua kutoa msaada huo ili kuwa sehemu ya jamii
iliyowasaidia wazee hao katika sikukuu ya Eid EL Fitri ili nao waweze
kusheherekea sikukuu hiyo bila kuwepo kwa vikwazo vya aina yoyote ile.
No comments:
Post a Comment