Habari za Punde

Jumuiya ya Istiqaamah Zanzibar wakabidhi msaada wa fedha kwa wananchi walioathirika na upepo Tumbatu

 WAFANYAKAZI wa Jumuiya ya Istikama Zanzibar wakiwa kwenye Boti wakielekea katika Kijiji cha Tumbatu kwaajili ya kukabidhi  Msaada wa fedha kwa Wananchi waliopatwa na Maafa ya Upepo hivi karibuni.
 MWENYEKITI wa kitengo cha Maafa  Jumuiya ya Istikama Zanzibar Said Hemed Alshaybar  akimkabidhi Msaada wa Fedha Bi. Dawa Jabiri Haji mkaazi wa Tumbatu Uvivini.
 MKURUGENZI Mtendaji Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Makame Khatibu Makame akimkabidhi Msaada wa fedha  Makame Mdungi Makame mkaazi wa Shehiya ya Bomani Tumbatu.
  MWENYEKITI wa kitengo cha Maafa  Jumuiya ya Istikama Zanzibar Said Hemed Alshaybar  akizungumza na Wananchi wa Tumbatu baada ya kukabidhi Msaada wa fedha kwa  waliopatwa na Maafa.
 SHEHA wa Shehiya ya Uvivini Hassan Muhidini akitoa shukurani kwa niaba ya Masheha wa Shehiya tatu za Tumbatu kwa Jumuiya ya Istikama baada ya kuwapatia Msaada kwa Wananchi waliopatwa na Maafa hivi karibuni.


Picha na Abdalla Omar  Maelezo - Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.