Habari za Punde

Programu ya 'UNI LIFE CAMPUS' Yafanikisha Ndoto za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania.

Mwanzilishi wa programu ya 'Uni Life Campus' Mbunge wa Viti Maalum Mheshimiwa Esther Mmasi ambaye anawakilisha Vyuo Vikuu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na wanafunzi wa vyuo mbali mbali vya Tanzania wakati wa semina elekezi juu ya kuzitunza fursa wanazozipata katika maisha yao ikiwa ni pamoja na kupatiwa nafasi za kufanya mafunzo kwa vitendo (field) katika taasisi mbali mbali za serikali na mashirika binafsi mwishoni mwa wiki iliyopita katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es Salaam. Picha zote na Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Mkurugenzi DM Saikolojia Limited Bw. Dosi Said Dosi akitoa neno kwa wanafunzi wanaotarajia kuanza mafunzo yao kwa vitendo (field) wakati wa semina elekezi juu ya kuzitunza fursa wanazozipata katika maisha yao katika taasisi mbali mbali za serikali na mashirika binafsi mwishoni mwa wiki iliyopita katika Chuo cha CBE jijini Dar es Salaam.. Meza kuu wakifuatilia kwa makini.
Mmoja ya maofisa katika Programu ya 'Uni Life Campus' Gladness akitoa maelezo machache kwa wanafunzi.
Rais wa Wanafunzi, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Said Hamisi Suba akitoa shukrani zake.
Mratibu wa Programu ya 'Uni Life Campus' Elibariki Abel akitoa muongozo wa masuala mbali mbali kwa wanafunzi.
Mwanafunzi Agustino wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) akiuliza swali... Mwanafunzi Abdulatif wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es Salaam akiuliza swali.
Mhe. Esther Mmasi (katikati mwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa vyuo mbali mbali waliohudhuria katika semina elekezi mara baada ya kupatiwa nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo (field) katika taasisi mbali mbali za serikali na mashirika binafsi mwishoni mwa wiki iliyopita Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.