




Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .
SHIRIKA
la Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeingia mkataba na Benki za Azania,NMB na
NBC kwa ajili ya utoaji wa mikopo kwa wanachama wake watakao ingia
kwenye mpango wa Hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi, lengo likiwa ni
kupunguza hali ya umaskini.
NSSF
imeanza utekelezaji wa mpango huu baada ya maboresho ya sheria namba 2 ya mwaka
2018 iliyotoa majukumu kwa shirika hilo kuboresha na kushuhulikia sekta isiyo
rasmi ambayo inatajwa kuwa kwa muda mrefu imetelekezwa.
Katika kuhakikisha elimu hii ya inawafikia
wananchi wengi ,NSSF imeanza kufanya mafunzo kwa viongozi wa vikundi vya
wajasiriamali ili kutoa hamasa na baadae kuwaingiza katika Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii wananchi wote ambao wako kwenye sekta isyo rasmi..
Mgeni rasmi katika semina hiyo
iliyofanyika katika ukumbi wa NSSF mjini Moshi,Kaimu Mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro ,Kippi Warioba akatumia nafasi hiyo kutoa rai kwa baadhi ya viongozi
wa vyama vya ushirika kuacha tabia ya ubadhirifu.
Kwa upande wao washiriki wa Semina
hiyo wakiwemo viongozi wa Benki zilizoingia mkataba na NSSF katika kuboresha
utoaji wa mikopo kwa wanachama walio kwenye sekta isiyo rasmi wakiwemo
wajasiliamali wadogowadogo wameelezea matumani yao juu ya mpango huo wa NSSF.
Wanachama ambao watanufaika na mpango
huu ni wale watakao toka kwenye vikundi vyenye sifa za mikopo ambayo
itasimamiwa na Benki ya Azania zikiwemo Saccos na Amcos zaidi ya 100.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment