Habari za Punde

Raia wa Iran Avunja Rekodi ya Miaka 19 Kwenye Mashindano ya Asia

Mwanamichezo kutoka Nchini Iran mnyanyua Vitu Vizito  Moradi alinyanyua kilo 189 kwenye kundi la kilo 94 la  wanaume na kuvunja rekodi ya kilo 188.

Raia wa Iran Sohrab Moradi amevunja rekodi ya kunyanyua uzani ambayo imekuwepo kwa miaka mingi na kushinda dhahabu kwenye mashindano ya Asia.
Moradi alinyanyua kilo 189 kwenye kundi la kilo 94 wanaume na kuvunja rekodi iliyokuwa imewekwa ya kilo 188 na Mgiriki Akakios Kakiasvilis mwaka 1999.
Fares Elbakh wa Qatar alichukua fedha huku Sumpradit Sarat wa Thailand akishinda shaba.
"Nilitaka sana kuvunja rekodi ya dunia kwa sababu ndiyo sikuwa nayo ni hii ilikikuwa fursa yangu ya mwisaho," alisema Moradi.
2Nina furaha sana kwa sababu jina langu litabaki kwenye rekodis za uzani wa kilo94."

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.