Habari za Punde

Rais Dkt Magufuli ampokea Waziri wa Maliasili na Utalii uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kutokea mkoani Arusha

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere kumshusha kutoka kwenye ndege  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara. Ndege hiyo iliwasili majira ya jioni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumpokea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika  ajali ya gari mkoani Manyara.
 Ndege maalumu iliyombeba Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere  kutokea mkoani Arusha majira ya jioni.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akisubiri kumpokea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alipata ajali ya gari mkoani Manyara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara mara baada ya kuwasili kwa ndege katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa ndani ya gari la wagonjwa kwa ajili ya kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.