Na.Mwandishi Wetu,
Ulanga.
SERIKALI
wilayani Ulanga mkoani Morogoro imesifu jitihada kubwa zinazo fanywa
na bodi ya Korosho Tanzania kwa kuwatembelea wakulima ili
kuwahamasisha umuhimu wa kulima kilimo chenye tija ili kuongeza
uzalishaji ikiwa ni mpango wa kuliendeleza zao hilo.
Hayo yalibainishwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Ulanga (DAS)
Abraham Mwaikwila wakati wakati wa ziara ya viongozi wa Bodi ya
Korosho iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kilimo hicho kwa wakulima
wilayani Ulanga ikiwemo upuliziaji wa dawa ili kuongeza
uzalishaji.
Viongozi wa
bodi ya Korosho ambao walikuwa kwenye ziara hiyo ya uhama sishaji huo
ni Afisa Habari wa Bodi ya Korosho Tanzania Bryson Mshana na Afisa
Kilimo Bodi ya Korosho Tanzania Frank Mfutakamba ambao walikutana na
wakulima wanaolima korosho wa kikundi cha Igombiro
Alisema kwamba wilaya hiyo tokea miaka ya nyuma walikuwa
wanalima korosho lakini baadae waliliacha kutokana na kutokuwa na soko
la uhakika lakini kwa sasa ili kuhakikisha zao hilo linalimwa kwa tija
mwaka jana walipewa ruzuku ya uzalishaji wa miche ya korosho laki tatu
ambayo waliigawa kwa wakulima.
“Sio hilo mikorosho ya zamani iliyokuwepo tulikuwa na
Mkurugenzi aliyekuwa akiitwa Isabela Chiluba aliyetoka Tandahimba
kwani baada ya kufika aliweza kuja na mwamko mzuri wa kufufua
mikorosho ya zamani kwa mfano mwaka jana walipata pembejo na kupulizia
mikorosho ya zamani jambo ambalo limefungua ukurasa mpya kwetu
“Alisema.
Alisema
kutokana na hilo mwaka huu wanatarajia kuzalisha miche kwa wingi hivyo
anaamini bodi ya korosho itakuwa na uhamasishaji mzuri na miche laki
tatu iliyotolewa kwa hiyo mwaka huu itakuwa chachu ya wananchi
kuhitaji miche utakuwa mkubwa sana.
Hata hivyo aliiomba bodi ya Korosho kuweka utaratibu wa kuwapa
miche ya korosho kutokana na kwamba asilimia kubwa ya mapato kwenye
Halamshauri ya Ulanga yanatokana na mazao hivyo anaamini Mkurugezi na
timu yake ya idara ya kilimo watajipanga kuhakikisha wanaenda kununua
mbegu kwenye vituo vya naindelee ili waweze kupata miche iliyobora na
kuwawezesha kuongeza uzalishaji wenye tija.
Naye kwa upande wake, Mratibu wa zao la Korosho wilaya ya
Ulanga mkoani Morogoro Samweli Masaro alisema kutokana na kuwepo kwa
uhamaishaji huo umewawezesha kuongeza uzalishaji kufikia tani
80.
Ambapo awali ulikuwa kwa
kiwango cha chini hali iliyowa ikiwalazimu kutilia mkazo uzalishaji wa
zao hilo kwa kuhamasishaji wakulima kulima ikiwemo kutunza miti yao na
kupiga dawa jambo ambalo kwa asilimia kubwa limesaidia kuweza
kuwawezesha kupata tani hizo ambazo pia wanatarajia huenda
zikaongezeka
No comments:
Post a Comment