Habari za Punde

Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mhe. Luhaga Mpina Atembelea Banda la Maonesho la Taasisi ya Pass Maonesho ya Nane Nane Mkoani Simiyu.

Muonekano wa Viwanja vya Nyakabindi ambako kunafanyika maonesho ya nane nane kitaifa mkoani Simiyu.
Waziri wa Uvuvi na Mifugo,Luhaga Mpina akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi Binafsi ya kusaidia Sekta ya Kilimo nchini (PASS) Nicomed Bohay wakati alipotembelea Banda la taaasisi hiyo lilipo katika viwanja vya nane nanemkoani Simiyu.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kusaidia Sekta Binafsi zinazojihusisha na masuala ya Kilimo,Uvuvi na Ufugaji ,(PASS) Nicomed Bohay akimuonesha Waziri wa Uvuvi na Mifugo,Luhaga Mpina mfano wa Bwawa linalotumika kufugia samaki ,Mabwawa ambayo Taasisi ya PASS imekuwa ikisadia katika upatikanaji wa mikopo kwa Wafugaji wa Samaki ili waweze kufuga kisasa.
Mmoja wa wanufaika wa  huduma zinazotolewa na Taasisi binafsi ya kusaidia sekta ya Kilimo nchini (PASS) ikiwemo ya unenepeshaji wa Ngombe  Michael Tegeshi akitoa maelezo kwa Waziri wa Uvuvi na Mifugo,Luhaga Mpina alipotembelea banda la taasisi hiyo katika maonesho ya nane nane yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi mkoni Simiyu.
Waziri wa Uvuvi na Mifugo,Luhaga Mpina akitizama Mchele uliowekwa vizuri katika mifuko kwa ajili ya kuongeza thamani ,Mchele huo unaandaliwa na vikundi ambavyo vimepata msaada kutoa katika taassi hiyo.
Meneja wa  PASS Trust  tawi la Mtwara ,Isaac Kileo akitoa maelezo kwa Waziri wa Uvuvi na Mifugo Luhaga Mpina alipotembelea banda la taasisi hiyo katika maonesho ya nane nane yanayofanyika kitaifa katika mkoa wa Simiyu
Waziri wa Uvuvi na Mifugo,Luhaga Mpina akimsikiliza Mkurugenzi wa Biashara PASS,Kilo Rusewa alipotembelea katika Banda la taasisi hiyo katika viwanja vya nane nane mkoani Simyu.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Prof Elisante Ole Gabriel akimuelekeza jambo Waziri wa Uvuvi na Mifugo ,Luhaga Mpina wakati akitembelea banda la Taasisi ya PASS katika maonesho ya nane nane mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akitizama Ng'ombe aliyenenepeshwa alipotembelea Banda la Taasisi ya PASS katika maonesho ya nane nane mkoani Simyu.
Baadhi ya Wananchi wakitizama Ng'ombe aliyenenepeshwa waliopo katika Banda la taasisi ya PASS katika maonesho ya nane nane mkoani Simiyu.
Meneja wa Biashara wa taasisi ya PASS ,Hamis Mmoni akizungumza na baadhi ya wananchi waliotembelea banda la taasisi hiyo katika maonesho ya nane nane yanayofanyika kitaifa mkoani Simiyu.
Baadhi ya wananchi wakitizama samaki katika moja ya bwawa la mfano lililopo katika banda la nane nane la taasisi ya PASS.

Sehemu ya mifugo iliyopo katika banda la maonesho ya nane nane la taasisi ya PASS  mkaoni Simiyu,

nA Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyeko Simiyu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.