Habari za Punde

Wananchi wa Kijiji cha Kitogani Waeleza Walivyonufaika na Mradi wa PAZA Zanzibar.

Na.Mwandishi Wetu.
Wakaazi wa Kijiji cha Kidogani Wilaya Kusini Unguja  wamesema wameondokewa na tatizo la maji safi na salama kupitia Mradi wa kukuza Uwajibikaji Zanzibar (PAZA) unaosimamiwa na Chama Cha wa Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Kwa upande wa Zanzibar, Waandishi wa Habari za Maendeleo (WAHAMAZA) na Jumuiya ya Uhifadhi wa Msitu wa Ngezi Pemba (NGENARECO).

Wakielezea kuhusu mradi huo Bi Khadija Kheri (58) amesema  huduma ya maji  imepatika  katika kijiji hicho baada ya Mradi wa PAZA kuwaelimisha  wananchi taratibu za kufuatilia  ufumbuzi wa matatizo katika  Ofisi ya Halmashauri za wilaya.

Amesema wakaazi wa kijiji cha Kitogani wamehamasiki kuibua matatizo kupitia mkutano mkuu wa kijiji ambapo wananchi wa jinsia zote walipata fursa ya kuzungumzia matatizo yanayowakabili  katika maeneo yao wanayoishi.

“Wananchi katika ule mkutano wamehahamishwa namna ya kuibua kero zetu zinazotukabili na wapi twende kuzidai na kutafutiwa ufumbuzi, kwa hivyo baada ya mkutano sisi kama wananchi tukenda kwenye ofisi za Halmashauri na kusema kero zetu na tunashukuru sasa tatizo la maji limetatuliwa” alisema.

Aidha Bi Khadija amesema jambo jengine kupitia mkutano huo wananchi waliibua changamoto nyingi ambazo zimetatuliwa ikiwemo kuboreshwa kwa hospitali ya Kitogani ambapo jengo la hospital hiyo lilikua limechakaa sana  pamoja ukosefu wa madaktari.


“PAZA imetuhamasisha na kutusaidia kujua haki zetu lakini pia imetusaidia jengo la hospitali sasa limejengwa vizuri ingawa hatujakabidhiwa lakini limeshafanyiwa ukarabati zuri limependeza na sio muda mrefu tumeahidiwa tutakabidhiwa” amesema Mama huo.

Khadija amesema wananchi wa Kijiji cha kitogani walikuwa wamekabiliwa na matatizo mengi ikiwemo la maji safi na salama, ukosefu wa walimu, huduma ya afya pia ilikuwa mbovu.

Kwa upande wake afisa afya wilaya kusini Jaku Ameir Issa amesema Ofisi hiyo itaendelea kuhakikisha kwamba wanawake wanapata huduma ya afya ya uzazi bure na madaktari  watapatikana wakati wote.

Amesema  Mradi wa PAZA umewawezesha wananchi wa kusini kuwajua maafisa wa serikali kwa ajili ya kuwaajibisha katika majukumu yao.

Akitoa takwimu za watu waliokwenda ofisini kwake alisema jumla wa watu wenye ulemavu 33, wanawake 42 na vijana 18 walifika ofisini kwake kupeleka maombi ya malalamiko ya kuomba kuboreshwa  huduma ya afya.

Mradi wa kukuza Uwajibikaji Zanzibar (PAZA) ulianza mwaka jana kwa lengo la kukuza Uwajibikaji Zanzibar ili kuwahamasisha wananchi njia za kutatua matatizo yanayozunguuka katika jamii na utarajiwa kumalizika mwakani.

Mradi wa Kukuza Uwajibikaji, Promote Accountability Zanzibar (PAZA) unafanya kazi katika shehia 14 za Unguja na Pemba kwa kushirikiana na Asasi za kiraia, Halmashauri na wana mitandao na unasimamiwa na ZANSAP na kufadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya, European Union (EU)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.