Habari za Punde

Michuano ya Kombe la Mapinduzi Kati ya Yanga na Azam. Timu ya Azam Imeshinda Bao. 3 -0.Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Mshambuliji wa Timu ya Azam akijaribu kuwapita wachezaji wa Timu ya Yanga wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Timu ya Azam imeshinda bao 3-0.
Wachezaji wa Timu ya Yanga na Azam wakiingia Uwanja kuaza mchezo wao wa Kunia Kombe la Mapinduzi 2019, mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Azam imeshinda mchezo huo kwa bao 3-0. 
Kikosi cha Timu ya Yanga kinachoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar kilichokubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Timu ya Azam, katika mchezo wao wa Pili wa Michuano hiyo mchezo wa Kwanza wamefanikiwa kushinda bao 1-0 dhidi ya Jamuhuri uliofanyika juzi. 
Kikosi cha Timu ya Azam kinachoshiriki Kombe la Mapinduzi kilichotowa kipigo kwa Timu ya Yanga kwa bao 3-0, ikiwa ni mchezo wake wa Pili wa michuano hiyo mchezo wa kwanza ilitoka sare na Timu ya Jamuhuri kwa bao 1-1. 
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.