Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala Pa Kazi Yaadhimishwa Mkoani Mbeya.





Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiwa pamoja na Naibu wake Mhe.Anthony Mavunde (wa kwanza kulia) na wa kwanza kushoto ni katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Andrew Massawe wakitembea katika viwanja vya Bustani ya Jiji wakati wa kukagua mabanda ya maonesho katika kuadhimisha Siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Aprili 28, 2019 yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Mbeya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipokelewa na watumishi wa OSHA alipowasili katika viwanja vya bustani ya Jiji Mkoani Mbeya kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika mkoani hapo kitaifa.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi Bi. Khadija Mwenda akieleza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama wakati wa maaadhimisho hayo, wa kwanza kushoto ni Naibu wake Mhe. Anthony Mavunde.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipewa maelezo ya vifaa saidizi kazini kutoka kwa Mtaalamu kutoka Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) wakati wa maadhimisho hayo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiuliza jambo kwa wataalam kutoka Idara ya Kazi wa ofisi hiyo alipotembelea banda lao wakati wa maadhimisho ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika Jijini Mbeya.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni katika banda la maonesho la Wakala wa Afya na Usalama mahala pa Kazi (OSHA) wakati wa maadhimisho hayo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista pamoja na naibu wake Mhe. Anthony Mavunde wakiangalia mfano wa namna ya kuokoa mtu aliyepata madhara awapo kazini walipotembelea banda la MUST (Mbeya University of Science and Technology) wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Jijini Mbeya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista pamoja na baadhi ya viongozi wa TUGHE wakifurahia jambo wakati alipotembelea banda la TUGHE katika maonesho hayo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista akifuatilia takwimu za ajari zitokananazo na shughuli za uchimbaji katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu alipotembelea banda la ofisi hiyo kujionea namna wanavyofanya kazi wakati wa maadhimisho ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Mkoani Mbeya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista akihutubia wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya kilele maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika Jijini Mbeya
Sehemu ya wananchi wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho hayo Jijini Mbeya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista akifurahia pamoja na watumishi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita  (GGM) baada ya kuibuka washindi wa kwanza kwa kupokea tuzo nyingi kuliko washiriki wengine wa maonesho ya Siku Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika Jijini Mbeya.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.