Mwakilishi wa jimbo la Ole Mh. Mussa Ali Mussa akimkabidhi Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Nd. Mo’hd Nassor Salim vifaa vya michezo kwa ajili ya Skuli ya Ng’ambwa Msingi.
Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Nd. Mo’hd Nassor Salim akimkabidhi Mwalimu Mkuu Skuli ya Ng’ambwa Msingi Nd. Juma Amour Juma vifaa vya michezo kwa ajili ya Skuli yake.
Na
Ali Othman.
Mwakilishi wa jimbo la Ole Mh. Mussa Ali Mussa
amekabidhi vifaa vya michezo kwa Skuli ya Ng’ambwa msingi kutokana na kuonesha
mafanikio katika sekta ya michezo.
Makabidhiano ya vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na
jezi kumi na tano (15) na mipira miwili (2) yamefanyika leo katika Ofisini ya Afisa Mdhamin Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Amali Chake chake Pemba.
Akikabidhi vifaa hivyo Mh. Mussa amezitaka skuli
nyengine kuiga mfano wa skuli ya Ng’ambwa Msingi kwa kuwajenga wanafunzi
kimichezo ambapo ameongeza kwamba
michezo hujenga afya nahivyo kuimarisha mafanikio katika masomo.
Nae Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Amali Nd. Moh’d Nassor Salim akielezea shukran zake za dhati kwa Mwakilishi
huyo kwa juhudi zake anazozifanya katika kuunga mkono sekta ya elimu, amewataka
viongozi wengine kuiga mfano wa Mwakilishi huyo katika kusukuma mbele maendeleo
ya elimu kisiwani Pemba.
Wakati huo huo akikabidhi vifaa hivyo kwa Mwalimu
Mkuu Skuli ya Ng’ambwa Msingi Nd. Juma Amour Juma, Afisa Mdhamini amemtaka
Mwalimu huyo kuhakikisha kwamba vifaa hivyo vinatunzwa na kutumika ipasavyo kwa
maendeleo ya michezo katika skuli hiyo.
Nae mwalimu Juma akielezea Shukran zake za dhati kwa
kupokea vifaa hivyo ameahidi kwamba atendelea kusimamia ipasavyo majukumu yake
ikiwa nipamoja na kuhakikisha kwamba Skuli ya Ng’ambwa msingi inaendelea kupata
mafanikio katika sekta ya michezo na maendeleo ya elimu kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment