Habari za Punde

ZFA Yapitisha Katiba Mpya Kuelekea Uchaguzi Mkuu na Kubadilisha Jina Baada ZFA na Sasa Inaitwa ZFF.

Na Hawa Ally. ZANZIBAR
MKUTANO mkuu wa CHAMA cha Soka Zanzibar ZFA   umepitisha katiba mpya ya chama hicho bila kupingwa  ambayo itaanza kutumika rasmi katika shughulizi zote za soka la Zanzibar.
Mkutano mkuu huo ulifanyika kisiwani Unguja katika Ukumbi wa uwanja wa Amaan huku ukihudhuliwa na wajumbe 9 kati ya 10 wa mikoa mitano ya Zanzibar.
Wajumbu hao waliopitisha katiba hiyo ni Wenyeviti   na Makatibu wa Mikoa yote ya Unguja na Pemba
Katika upitishwaji wa katiba huo wajumbe tisa  waliokuwepo ukumbini hapo  walikubali kupitisha katiba hiyo huku mjumbe mmoja kutoka mkoa mjini Magharibi hakuhudhukiwa kutokana na matatizo ya kiafya na  aliwasilisha kwa njia ya maandishi ikifanya katiba hiyo kupita bila kupingwa.
Katiba hiyo ambayo sasa inaiiyondoa jina la Chama cha Soka ZFA na kuwa shirikisho la Soka Zanzibar ZFF  ili kuweza kufikia malengo ya kukuza soka la Zanzibar katika ngazi zote kuanzia chini.
Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kumalizika mkutano huo katibu wa Chama hicho ambapo kwa  sasa  shirikisho  Mohamed Ali alisema mchakato unaofata hivi sasa ni kuweza kufanya uchaguzi mkuu wa chama hicho kupitia katiba hiyo mpya ambapo imepitishwa hii leo.
Alisema punde  kamati ya uchaguzi itakapotangzwa na wao watakuwa na jukumu la kushugulikia taratibu hizo za uchaguzi wa Rais, Makamu na wajumbe wa kamati Tendaji.
Aidha  akizungumzia katiba hiyo mpya alisema katiba hiyo imeweka mambo mengi yatakayochangia kukuza soka la Zanzibar pamoja na kwenda na Wakati kama mashirikisho mengine ya soka.
Alisema miongoni mwa mambo muhimu kabisa ni kupiga hatua ya kuitwa ashirikisho jambo ambalo linahitaji jitahada kubwa ili tuweze kufikia lilelengo la jina hilo ikiwemo kuwa na soka bora na litakalotoa wachezaji wazuri ambao wataweza hata kuiwakilisha Zanzibar nje ya Zanzibar.
“Katiba hii inamambo mengi ambayo yatapeleka soka letu mbele kuanzia kanzi ya chini kabisa, kikubwa viongozi watakaochaguliwa waifate na wahakikishe kile ambacho kilichopendekezwa katika katiba kinafanyiwa kazi”Alisema.
Hata hivyo katiba hiyo imeandikwa kwa lugha ya kingereza hivyo katibu huyo alifahamisha kuwa wapo katika mchakato wa kuitafsiri katika lugha ya Kiswahili kwa hara ili wadau wa soka wasioelewa klugha hiyo waweze kuisoma kupitia lugha yetu ya Taifa Kiswahili.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.