Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Azungumza na Uongozi wa Wizara ya Ardhi Nyumba Maji na Nishati Zanzibar.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ardhi Nyumba Maji na Nishati Zanzibar, kuzungumzia Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara hiyo kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Marchi 2019. mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.

Rais Dk. Shein alikutana na uongozi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati chini ya Waziri wake Salama Aboud Talib ambapo katika taarifa ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara hiyo kwa kipindi cha Julai 2018 hadi Machi 2019 alieleza kuwa Mikakati ya Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za maji, nishati iliyosalama na endelevu, makaazi bora na matumizi mazuri ya ardhi.

Alisema kuwa Wizara hiyo kupitia Mamlaka ya Maji (ZAWA), imeendelea kusimamia shughuli za program za uhuishaji na upanuzi wa shughuli za maji mijini na vijijini.

Kwa upande wa ujenzi wa jengo la Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA), Waziri Salama alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo unaendelea kwa kasi ya kuridhisha na hadi kufikia Machi 2019 jengo limekamilika kwa asilimia 60.

Waziri salama alieleza hatua zilizofikiwa katika utiaji saini Mkataba wa Kwanza wa Mgawanyo wa Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia uliofanyika Oktona 23, 2018 huku akieleza jinsi Serikali inavyoendelea na azma yake ya kutumia nishati mbadala ya jua.
  
Nae Rais Dk. Shein kwa upande wake alieleza haja kwa Wizara hiyo katika kuzisimamia vyema taasisi zake hasa kwa kutokana na kubeba mahitaji mengi ya wananchi huku akitumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa Wizara hiyo kwa kutekeleza vyema majukumu waliyopewa.

Aidha, Rais Dk. Shein alisisitiza haja kwa uongozi wa Wizara hiyo kutoa elimu kwa wananchi hasa juu ya umiliki wa ardhi kwani asilimia kubwa ya wananchi hawafahamu sharia za umiliki wa ardhi.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.