Habari za Punde

Chiba FC na Lion Kids zashindwa kutambiana kombe la Kipwida

Na Mwajuma Juma

TIMU za soka za Chiba FC na Lion Kids zimeshindwa kutambiana katika michuano ya kombe la Kipwida inayoendelea kwenye viwanja vya Maungani.

Mchezo huo ambao ni wa pili kufanyika ulichezwa majira ya saa 10:00 za jioni kushuhudiwa wanaume hao kutoka sare tasa licha ya kuwepo kwa mashambulizi ya kasi uwanjani hapo.

Wakicheza kwa kuanza taratibu mchezo huo miamba hiyo ilikwenda mapumziko wakishindwa kufungana na kipindi cha pili kilipoanza wakajikuta matokeo hayakuweza kubadilika.
Kocha wa timu ya soka ya Lion Kids Mwinyi Shego Mohammed amesema kuwa sare ni moja ya matokeo ya mchezo kati ya matokeo matatu yanayotokana katika mpira wa miguu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya mchezo kati yake na timu ya Chiba FC ambao walitoka sare ya kutokufungana alisema kuwa  mchezo ulikuwa mzuri lakini umaliziaji wake kwa wafungaji wake ndio uliokwanza kutokupata mabao.

“Kwangu mimi kilichonifanya nishindwe ni masuala ya ufungaji tu lakini sare ni moja ya matokeo ya mchezo”, alisema.

Alisema kuwa wachezaji wake walijitahidi kulenga mashambulizi langoni mwa wapinzani wao na kuonekana kuumiliki sana lakini umaliziaji ulikuwa butu.

“Kiujumla mchezo huu utuliutawala kila idara na kila mmoja ameshuhudia lakini tatizo letu ni umaliziaji tu ambalo kama mwalimu tunajipanga kuona tunalifanyia kazi”, alisema.

Hata hivyo alisema kuwa katika mchezo ujao anauhakika suala la umalizijaji litakuwa mwiko na kutarajia kupata mabao mengio ya kufunga.

Ligi hiyo leo inatarajiwa kuendelea tena kwa kupigwa mchezo mmoja utakaowakutanisha Uzi FC na Makunduchi Kids.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.