Kaimu Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN), ambaye pia ni Meneja Masoko na Mauzo, Bw, Januarius Maganga(wapili kulia), akizungumza jambo na Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, (wakwanza kushoto), wakati alipotembelea kampuni hiyo jijini Dar es Salaam Juni 11, ikiwa ni ziara ya kujenga mahusiano lakini pia kueleza shughuli za Mfuko huo ambao umeanza kutekeelza majukumu yake Agosti 2018 baada ya serikali kuiunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF, LAPF, PPF na GEPF.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
JUMLA
ya wastaafu elfu 10,500 bado hawajafika kwenye ofisi za Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), ili kuhakiki taarifa zao hadi sasa, Meneja
Kiongozi Uhusiano wa Mfuko huo Bi. Eunice Chiume ameyasema hayo kwa nyakati
tofauti wakati akitembelea vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo Juni 11,
2019.
Vyombo vya habari alivyotembelea leo Juni 11, 2019 kwa lengo la kujenga mahusiano na kueleza shughuli za Mfuko huo ambao ni Mpya ni pamoja na magazeti ya serikali yanayomilikiwa na kampuni ya Tanzania Standard News Papers (TSN), Azam Media, wamiliki wa Azam TV na Uhai FM, Mwananchi Communications Limited, wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, Citizen na Mwanaspoti na Clouds Media Group, wamiliki wa Clouds TV na Clouds FM.
Alisema,
zoezi la kuhakiki taarifa za wastaafu huwa linafanyika kila mwaka na huu ni
utaratibu wa taasisi za hifadhi ya jamii na kwa upande wa PSSSF zoezi lilianza
Desemba mwaka jana (2018).
”Tangu
Mfuko huu uanze shughuli zake Agosti 1, 2018 PSSSF ilifungua ofisi nchi nzima Bara
na Visiwani na hivyo tunatoa wito kwa wastaafu wote ambao bado hawajahakiki
taarifa zao kufanya hivyo kupitia ofisi zetu zilizoenea nchi nzima na wala hawalazimiki
kuja makao makuu Dodoma kupatiwa huduma hiyo. “Alifafanua Bi. Eunice Chiume.
Zoezi
la kuhakiki taarifa hufanyika kila mwaka kwa upande wetu tulianza zoezi hili
Desemba mwaka jana (2018) na liliendelea hadi Machi 2019 na tumeanza tena na
zoezi hilo nab ado linaendelea.
“kuhakiki
taarifa ni muhimu kwani kunasaidia kujiridhisha na taarifa za wastaafu wetu kwa
sababu huwa kunakuwa na mabadiliko mbalimbali ikiwa ni pamoaja na kujua kama
bado wapo, au taarifa zao za kibenki zimebadilika au la nah ii inasaidia
kufanya malipo sahihi na kwa mtu sahihi.” Alibainisha.
Meneja
huyo Kiongozi alitoa wito kwa wastaafu na jamii kwa ujumla kuwa PSSSF iko imara
katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wastaafu na wanachama wake wote
popote pale nchini. “Mafao yenu yapo wastaafu wote, nendeni mkahakik taarifai,
na hata ndugu ambao ndugu zao wastaafu ni wagonjwa wafike kwenye ofisi zetu na
sisi tutakwenda kufanya uhakiki huko huko aliko.” Alifafanua Bi. Enice Chiume
ambaye anaendelea na ziara yake Alhamisi Juni 12, 2019.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, (wakwanza kushoto), akiwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi (wapili kushoto), wakiwa kwenye mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya magazeti ya serikali (TSN), chini ya Kaimu Mhariri Mtendaji, Bw. Januarius Maganga (wakwanza kulia), ikiwa ni muendelezo wa ziara ya meneja huyo kiongzi kutembeela vyombo vya habari kwa nia ya kujenga mahusiano na kueleza shughuli za Mfuko huo mpya.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, akifafanua masuala mbalimbali kuhusu shughuli na majukumu ya Mfuko huo.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, akifafanua masuala mbalimbali kuhusu shughuli na majukumu ya Mfuko huo.
Kaimu Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN), ambaye pia ni Meneja Masoko na Mauzo, Bw, Januarius Maganga, akizungumza mbele ya mgeni wake Bi. Eunice Chiume wakati wa mazungumzo yao
Picha ya pamoja na uongozi wa TSN.
Picha ya pamoja |
Mhariri Mtendaji wa gazei la Mwananchi, Bw. Frank Sanga (kulia), akiongozana na Bi. Eunice Chiume, wakati alipotembelea chumba cha habari cha kampuni ya Mwananchi Communications Tabata jijini Dar es Salaam Juni 11, 2019.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa PSSSF, Bi. Eunice Chiume, (wapili kushoto) na Bw. Abdul Njaidi (watatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi cha XXL, cha Clouds FM, kutoka kushoto, B12, Kennedy the Remedy, na DJ
Picha ya pamoja na uongozi wa Clouds Media
No comments:
Post a Comment