Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.
Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na
wanariadha walioshiriki mbio za Capital City Marathon (hawapo pichani) kwa
niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluh
Hassan zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.Kulia ni mratibu wa mbio
hizo Bw.Nsolo Mlozi na Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi,Ajira,Vijana na wenye ulemavu Mhe.Antony Mavunde.
Na Shamimu Nyaki –WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe ametoa pongezi kwa watanzania kwa kuwa na mwamko
mkubwa wa kupenda michezo kuanzia kushiriki,kushangilia pamoja na uhamasishaji
ambao umechangia kwa kiasi kikubwa
mafanikio na maendeleo ya michezo
hapa nchini na uwakilishi mzuri nje ya nchi.
Dkt.Mwakyembe ameyasema hayo leo Jijini Dodoma
alipokuwa anamuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe.Samia Suluh Hassan katika mashindano ya riadha ya Capital City Marathon
ambapo amesema kuwa kwa sasa nchi yetu imeanza kurudi katika ramani ya michezo
kutokana na watanzania kushriki kwa wingi katika michezo mbalimbali.
“Nawapongeza sana Watanzania wamekuwa na ari kubwa
sana ya kushirikiki michezo hasa riadha ambayo imetutangaza vyema nje ya
nchi,ni matuamini yangu mtaendelea kufanya vizuri zaidi lakini pia na michezo
mingine vijana endeleeni kuchezakwa bidii zaidi
kwakua michezo sasa ni chanzo kikubwa cha kipato”amesema Dkt.Mwakyembe.
Aidha Dkt.Mwakyembe ameongeza kuwa Taifa limekuwa
na uwakilishi mzuri katika mchezo wa Soka kwani limepata nafasi ya kushiriki
AFCON 2019,kuongezeka kwa timu zitakazoshiriki Klabu Bingwa Afrika ambayo ni
Simba na Yanga pamoja na Klabu Mbili zitakazoshiriki Kombe la Shirikisho ambazo
ni Azam FC na KMC.
Katika hatua nyingine Mhe.Waziri Mwakyembe
ameiagiza Idara ya Maendeleo ya Michezo kushirikiana na wadau kuwa na utaratibu
wa kuandaa orodha ya wadhamini wanaojitokeza
na namna wanavyodhamini mashindano mbalimbali ili kuweka kumbukumbuku vizuri na
kutoa ushauri panapowezekana katika kuimarisha Sekta hiyo.
Kwa upande wake Mratibu wa Mbio hizo Bw.Nsolo
Mlozi mbali na kuishukuru Serikali kwa ushirikiano iliyotoa pamoja na washiriki
waliojitokeza ameishauri jamii kuwa na
utaratibu wa kufanya mazoezi na kushiriki mashindano mbalimbali ya riadha ili
kujenga miili yao kwa kuimarisha afya lakini pia kujikinga na magonjwa
yasiyoambukiza ambayo kwa sasa yamekuwa yakiwatesa wananchi wengi.
Vilevile Bw.Nsolo ameongeza kuwa Capital City
Marathon ilianza na kuwa na idadi ndogo ya washiriki lakini mwaka huu idadi imeongezeka na kufikia
washiriki 2,200 ambao kulingana na miundombinu imara ya Jiji la Dodoma wameweza
kukimbia bila kupata changamoto yoyote.
Naye mshindi wa km 21 kwa upande wa wanaume Bw.Emmanuel Giniki amesema kuwa mchezo wa
riadha ni mchezo ambao unahitaji kuwa na mazoezi ya mara kwa mara ili kuweza
kufanya vizuri ambapo amewashauri vijana wengi kujitokeza katika mashindano
mbalimbali ya riadha yanayotokea ili kupata kipato pamoja na kupata ajira.
Mbio za Capital City Marathon zinafanyika kwa mara
ya pili Jijini Dodoma ambapo mwaka huu zimehusisha mbio za KM 22 Baiskeli,km.21wanawake
na wanaume,km 10 wanawake na wanaume pamoja na km 5.
No comments:
Post a Comment