Habari za Punde

Wazee Sebleni na Welezo wapatiwa mafunzo ya kukabiliana na maafa

 Mkuu wa Kamisheni ya kukabiliana na maafa Zanzibar Ali Faki Hamdani akitowa elimu kwa Wazee jinsi ya kujikinga na maafa huko kituo cha kulelea Wazee Sebleni.
 Mkufunzi kutoka Kamisheni ya kukabiliana na maafa Zanzibar Ali Haji Khamis akitoa mafunzo ya vitendo ya kumpatia huduma ya kwanza mzee Mohamed Said Abdalla huko katika Kituo cha kulelea Wazee Sebleni.
 Baadhi ya Wazee wa kituo cha kulelea wazee Sebleni na Welezo wakifuatilia kwa makini mafunzo ya kumpatia Mgojwa huduma ya kwanza

 Picha na Khadija Khamis Idara ya Habari Maelezo Zanzibar  

Baadhi ya Wazee wa kituo cha kulelea wazee Sebleni na Welezo wakifuatilia kwa makini mafunzo ya kumpatia Mgojwa huduma ya kwanza
 Picha na Khadija Khamis Idara ya Habari Maelezo Zanzibar  

Na Khadija Khamis - Maelezo Zanzibar            
Mkuu wa Kamisheni ya kukabiliana na maafa Zanzibar Ali Faki Hamdani amewataka Wazee kuzima vifaa vinavyotumia umeme hasa wakati wa kulala usiku ili kujiepusha na majanga yanayoweza kujitokeza.
Hayo aliyasema huko katika kituo cha kulelea Wazee Sebleni wakati akitoa mafunzo kwa wazee na wafanyakazi wa kituo hicho.
Amesema Wazee hao wanapaswa kuchukuwa tahadhari na vitu vyote hatarishi kama vile Mishumaa na vifaa vya umeme na kuwaomba kuvizima hasa kwa vile umeme hautabiriki.
Aliwataka  wafanyakazi wa vituoni  vya kulelea Wazee wawe na uangalizi mzuri kwa wazee hao kwani wanahitaji  tahadhari ya kulindwa kutunzwa na kuwekewa hadhari  kwani baadhi ya wazee wenye umri mkubwa akili zao hurudi nyuma.
Mkuu huyo alisema majanga ni tukio lolote ambalo linaweza kupelekea maafa kwa kuweza kuhatarisha maisha ya watu wengi kwa muda mchache kama vile majanga ya moto, Sunami, Matetemeko ya Ardhi na mafuriko.
Aidha alifahamisha kuwa mafuriko hutokea pale njia za kupita maji zinapozibwa ama wananchi kujenga sehemu zenye mito na mabwawa ya maji kipindi cha mvua kubwa.
Alifahamisha  kuwa maafa ya kimaumbile hutokezea ghafla na kusababisha vifo na upotevu wa mali  hivyo ni jambo jema kwa  wazee kupewa elimu na njia za kujikinga.
Nae Mkuu wa Kitengo cha Elimu na Ushauri Nasaha kutoka Kamisheni ya kukabiliana na maafa Haji Ame Haji amewataka wazee kuyatekeleza kwa vitendo pindipo yakitokea na kuwasaidia wenzao  .
Alifahamisha elimu ya kujikinga na maafa ni muhimu hasa kwa Wazee ambao wanahitaji kujua namna ya kujihami na kujiwekea tahadhari katika shughuli zao za kila siku
Mafunzo hayo ya Kukabiliana na Maafa kwa Wazee yametolewa na Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa chini ya Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.