Habari za Punde

ZSSF Imetiliana Saini ya Makabidhiano ya Jengo Lililokuwa Hoteli ya Mkoani Kisiwani Pemba.

Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko wa Jamii Zanzibar ZSSF Bi. Sabra Issa Machano, akitiliana saini Mahiri Said Ali, Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Engineering Co.Ltd, itakayofanya matengenezo makubwa na kuongeza ghorofa mbili za jengo hilo na uwekaji wa samani zote za hoteli.  
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF, inatarajia kutumia shilingi bilioni 11, kwa ajili ya ujenzi wa afisi za ZSSF Pemba pamoja na kulifanyia matengenezo makubwa jengo la Hoteli ya Mkoani, ili liweze kutoa huduma kama ilivyo kuwa maika 45 iliopita.
Kwani matengenezo ya Hoteli hyo, ambayo zamani ikijulikana kama hoteli ya SMZ, ilifunguliwa Januari 9, mwaka 1974, ingawa kwa miaka zaidi ya 12 sasa ilisitisha kutoa huduma za hoteli kwa wananchi na wageni.
Ndio maana ZSSF, baada ya kukabidhiwa jengo hilo Oktoba 9, mwaka 2018 na Wizara ya Fedha na Mipango, hapo mwaka jana, sasa imeshajipatia fedha shilingi bilioni 4 kwa ajili ya ukarabati, ili baadae itowe huduma za hoteli na kualaza wageni kama ilivyokuwa zamani.
Ukarabati huo  mkubwa wa jengo hilo ambalo kwa sasa lina ghorofa moja, utahusisha kuongeza ghorofa mbili na kufikia vyumba 14 kutoka vinane vya sasa.
Baada ya matengenezo hayo, hoteli hiyo ya ZSSF Mkoani itakayokuwa ya ghorofa tatu, itakuwa na vyumba vya wageni mashuhuri, ukumbi wa mikutano unaochukua watu 100 kwa wakati mmoja.
Pamoja na ukarabati huo, pia ZSSF kwenye hafla iliofanyika uwanja wa kufurahishia watoto wa Tibirinzi Chakechake, chini ya Mkurugenzi Mwendeshaji Sabra Issa Machano, alitiliana saini ujenzi wa jengo jipya la afisi za ZSSF Pemba.
Katika hafla hiyo  ya utiaji saini, iliohudhuriwa na viongozi wa wizara ya fedha, Bodi ya wadhamini na uongozi wa ZSSF, sambamba na wakuu wa wilaya, makatibu tawala, maafisa wadhamini, kamati za ulinzi na usalama, ambapo ZSSF iliwakilishwa na Mkurugenzi mwendeshaji katika utaiji wa saini hiyo.
Ambapo kampuni ya Quality Building LTD, iliowakilishwa na Mkurugenzi mtendaji Khamis Ali Shaibu imetia saini na ZSSF kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za ZSSF Pemba, huku kampuni ya Benchmark Engeneering iliowakilishwa na  Mkurugenzi wake Mahir Said Ali, watalifanyia ukarabati mkubwa jengo la ZSSF la Hoteli ya Mkoani.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa hafla hiyo, Mkurugenzi Mwendeshaii wa ZSSF Sabra Issa Machano, alisema mradi wa ujenzi jengo la afisi, ni katika jitihada za ZSSF za kuweka fedha za ziada katika miradi yenye tija.
Alisema jengoi hilo, ambalo litakuwepo upande wa kaskazini Mashariki nje ya kiwanja cha kufurahishia watoto cha Tibirinzi Chakechake, litakuwa jengo la ghorofa tatu.
Alisema baada ya kampuni ya Quality Building kushinda zabuni, ndio itakayojenga jengo hilo ndani ya miezi 12 chini ya kampuni ya Arqes Africa ya jijini Dar- es Salaam.
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa, pamoja na kuwapa nafasi nzuri watendaji wao, lakini pia ni kuzidi kupanua huduma zao sambamba na wanachama wa mfuko, ambapo pia sehemu nyingine zitakodishwa kama afisi kwa taasisi.
“Kama hilo likifanikiwa kwa kuzikodisha na taasisi nyingine, ndio haswa ambapo itakuwa ni rahisi kuweza kurejesha fedha ambazo zitatumika kwa ujenzi,”alieleza.
Akizungumzia kuhusu ukarabati wa jengo la hoteli ya Mkoani, kazi itakayofanywa na Kampuni ya Benchmark Engineering, unatarajiwa kutumia shilingi bilioni 4, samba na uwekaji wa samani zote za hoteli.
Hivyo amewataka wajenzi wa mejengo hayo, kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati uliopangwa, na kuhamiwa kwa wakati.
Mapema Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, aliwataka wajenzi hao kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa majengo hayo.
Hata hivyo Mkuu huyo Mkoa, ameuhakikishia uongozi wa ZSSF kwamba hakuna jambo litakalo kwama, wakati huu wa ujenzi na ukarabati, na hata likitokezea watalitatua.
Alisema wa ukarabati huo wa hoteli, utafungua milango mengine mipya ya uchumi kisiwani Pemba, sambamba na kuzaa ajira za kudumu kwa wananchi has kwa upande wa Hoteli.
Alieleza kuwa, Mfuko wa ZSSF umekuwa ukiyaweka mazingira na maisha ya wananchi vizuri, kwa kuwekeza vitega uchumi kila eneo, jambo ambalo linaleta faraja.
“Mimi niwapongeza sana ZSSF kwa kuendelea kulitumikia vyema taifa hili, na maagizo ya serikali kuu kwa kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wote,”alieleza Mkuu huyo wa Mkoa.
Kwa upande wake Mwneyekiti wa Bodi ya ZSSF Dk Suleiman Rashid Mohamed, aliwataka wajenzi wa majengo hayom kuhakikisha wanatekeleza agizo lililomo kwenye mikataba ya kujenga majengo yenye ubora.
Mapema Mkuu wa wilaya ya Chakechake Rashid Hadid Rashd alisema anafarajika kuona wilaya yake imekuwa ikikua kimaendeleo siku hadi siku na hasa kupitia uwekezaji wa ZSSF.
Mfuko wa Hifadhi wa Jamii Zanzibar ZSSF umekuwa ukutumia fedha za wanachama wa mfuko kwa ajili ya uwekezaji, katika miradi yenye tija, ili baadae waweze kuzirejesha na wanachama wakabidhiwe wanapo stafaafu.
ZSSF ambao umeanzishwa kwa sheria no 2 ya mwaka 1998 na kufanyiwa marekebisho kadhaa na kuanzishwa upya kwa sheria no 2 ya mwaka 2005 baada ya mapitio makubwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.