Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Azungumza na Waombolezaji wa Vifo Vya Watu Waliofariki Dunia Katika Ajali ya Lori la Mafuta Morogoro.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waombolezaji  wakati aliposhiriki  katika maandalizi ya kutambua miili na maziko ya watu 69 waliofariki dunia katika ajali ya lori la mafuta lililopinduka na kushika moto  katika  eneo la Msamvu mjini Morogoro. Alizungumza na waombolezaji hao kwenye viwanja vya hospitali ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akitazama mahali ambapo lori la mafuta lilipinduka na kushika moto hatimaye kusababisha vifo vya watu 69 kwenye eneo la Msamvu mjini Morogoro wakati alipotembelea eneo hilo, 
Baadhi ya waombolezaji wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kushiriki katika maadalizi ya kutambua miili na mazishi ya watu 69 waliofariki dunia katika ajali ya lori la mafuta lililopinduka na kushika moto kwenye eneo la Msamvu mjini Morogoro. Alizungumza na waombolezaji hao kwenye viwanja vya hospitali ya mkoa wa Morogoro
Baadhi ya waombolezaji wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kushiriki katika maadalizi ya kutambua miili na mazishi ya watu 69 waliofariki dunia katika ajali ya lori la mafuta lililopinduka na kushika moto kwenye eneo la Msamvu mjini Morogoro. Alizungumza na waombolezaji hao kwenye viwanja vya hospitali ya mkoa wa Morogoro. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya Mawaziri na viongozi wa mkoa wa Morogoro walioshiriki katika maandalizi ya kutambua miili na maziko ya watu 69 waliofariki dunia katika ajali ya lori la mafuta lililopinduka na kushika moto kwenye eneo la Msamvu mjini Morogoro. Alikuwa  kwenye viwanja vya hospitali ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. Kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Morogoro, Innocenti Kalogelisi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe na kulia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.