Habari za Punde

Innalilahh Waina Rajuun Ndugu Yetu Ibrahim Rajab Juma Jeba.

 Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania  pia alichezea Timu ya Chuoni kabla ya kwenda Timu ya Azam na Mtibwa zote za Tanzania Bara.
Marehemu jeba alikuwa akipata matibabu katika hospitali ya Taifa ya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar alipokuwa akipata matibabu.
 Marehemu amefariki jioni hii katika Hospitali ya Taifa ya Mnazi Mmoja kwa mujibu wa ndugu wa marehemu. Anatarajiwa kuzikwa kesho Kijiji kwao Ndijani Wilaya ya Kati Unguja.
Maziko yataondokia nyumbani kwao magomeni Unguja kesho na kuzikwa Kijiji Kwao Ndijani Wilaya ya Kati.
Mauti yakimkuta alikuwa mchezaji wa Timu ya Chuoni inayoshiriki michuano ya Ligi Kuu ya Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.