Habari za Punde

Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum Zanzibar Wamaliza Ziara yao Kisiwani Pembe Kukagua Mashamba ya Serikali.

Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiekuwa na Wizara maalumu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Said Soud Said, akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kusini Pemba , chini ya Mwenyekiti wake , Mkuu wa Mkoa huo Hemed Suleiman Abdalla, katika kikao cha maujumuisho ya ziara yao ya kungalia mashamba ya eka yaliofichwa katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mkoa wa kusini Pemba. 
Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiekuwa na Wizara maalum wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Juma Ali Khatib, akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kusini Pemba, chini ya Mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa huo , Hemed Suleiman Abdalla, katika majumuisho ya ziara yao ya kuangalia mashamba ya eka yaliofichwa kikao ambacho kilifanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa kusini Pemba wakiwa katika kikao cha majumuisho ya ziara ya wajumbe wa baraza la Mapinduzi waliofika Pemba kuangalia mashamba ya eka yliofichwa na kutumiwa na watu wasiohusika kwa maslahi binafsi.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo , Hemed Suleiman Abdalla, akizungumza na Kamati hiyo na wajumbe wa Baraza la Mapinduzi katika kikao cha majumuisho ya Ziara ya Wajumbe hao ya kuangalia mashamba ya eka 3 yaliofichwa katika baadhi ya shehia za Mkoa huo katika kikao
kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi hiyo Chake Chake Pemba.
Picha na Bakari Mussa - Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.