Habari za Punde

Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mhe.Mgimwa Kusomesha Wanafunzi Kuazia Kidatu cha Tano Hidi Chuo Kikuu.

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akivalishwa skafu na mmoja ya wanafunzi wa shule ya sekondari Ifwagi wakati alipotembelea shule hiyo.


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ifwagi iliyopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wametakiwa kufaulu kwa kiwango cha kupata daraja la kwanza ili waweze kupata fursa ya kupata ufadhili wa kusomeshwa na Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa.

Akizungumza wakati alipotembelea shuleni hapo Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa alisema kuwa mwanafunzi atakayepata daraja la kwanza atamsomesha kwa kumlipia baadhi ya mahitaji muhimu kuanzia kidato cha tano hadi chuo kikuu.

“Mimi nipo tayari kuchangia baadhi ya mahitaji kwa wanafunzi watakao faulu vizuri katika mtihani wa mwisho wa kidato cha nne ambapo mnatarajia hivi karibuni mtafanya mtihani huo”alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kufanya hivyo kutaongeza chachu ya wananfunzi kusoma kwa bidii na kuwa na ufaulu ambao utaleta maendeleo ya mwanafunzi na shule yenyewe hivyo mnatakiwa kusoma kwa bidii na kuzingatia masomo yenu ili mpate matokeo mazuri ya mtihani wa mwisho.

Aidha Mgimwa alisema kuwa anaendelea kuboresha sekta ya elimu kwa kujenda mabweni katika shule mbalimbali za jimbo la Mufindi Kaskazini hivyo hata hapa Ifwagi tunaendelea na ujenzi wa bweni kwa lengo la kuhakikisha tunaboresha elimu na kukuza ufaulu kwa wanafunzi wa shule hii.

“Nimechangia fedha nyingi kwenye bweni lenu hili ambalo ndio kwanza tumeanza hivyo mtuombee kwa mungu ili tukamilishe ndoto ya ujenzi wa bweni hili na wanafunzi mnatakiwa kudhamini mchangao wa wazazi,walimu,mbunge wenu na serikali kwa ujumla kwa juhudi ambazo zinafanywa kuleta maendeleo” alisema Mgimwa”

Mgimwa aliongeza kwa kusema kuwa katika shule ya sekondari ya Ifwagi amechangia katika ujenzi wa vyoo,bweni,uchimbaji wa kisima pamoja na kushughulikia maswala ya michezo hivyo rai yake kwa wanafunzi ni kuhakikisha wanasoma kwa bidii ili yapatikane matokeo mazuri.

Naye afisa elimu sekondari wilaya ya Mufindi Musa Ally alimpongeza mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kwa juhudi anazozifanya kuhakikisha anaboresha sekta ya elimu kwa kuchangia kila mara kwenye shule zote zilizopo katika jimbo hilo.

“Huyu mbunge amekuwa msaada sana kwetu maana kila mara tukiomba msaada wowote unahusu elimu amekuwa akitusaidia kwa hali na mali ni tofauti na wabunge wengine hivyo mnapaswa hata kuwaambia wazazi wenu mchango wa mbunge huyu kwenye sekta ya elimu” alisema Ally


Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo ya sekondari ya Ifwagi walimpogeza mbunge huyo na kumuomba aendelee kuwasaidia kuboresha elimu kwa kuwa elimu ndi msingi mkuu wa maisha ya mwanadamu.

Afisa elimu sekondari wilaya ya Mufindi Musa Ally akiongea na wanafunzi wakati wa ziara ya Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa shuleni hapo
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari Ifwagi alipofanya ziara ya kikazi katika shule hiyo
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa sambamba na afisa elimu sekondari wilaya ya Mufindi Musa Ally na mtendaji wa kata ya Ifwagi wakati wa ziara ya mbunge huyo katika shule hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.