Habari za Punde

Walimu Maskuli watakiwa kujiepusha na kuhubiri siasa


na Takdir Suweid, Wilaya ya Mjini.            

Naibu waziri wa nchi Ofisi ya Raisi,Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Ibara maalum za SMZ Shamata Shaame Khamis amewataka waalimu kuwacha kuhubiri siasa kwa wanafunzi wao na badala yake wasomeshe kwa kufuata mitaala iliowekwa na Wizara ya elimu.

Mh.Shamata ameyatoa hayo huko Skuli ya Msingi Kisiwandui wilaya ya Mjini katika hafla ya kuwapa zawadi Wanafunzi waliofaulu michipuo ya darasa la  la sita katika skuli hiyo.

Amesema kuna baadhi ya Waalimu wanakwenda kinyume na Taratibu za Ualimu kwa kuwafundisha Wanafunzi masuala ya yasiofaa jambo ambalo linaweza kusababisha Wanafunzi hao kukosa uzalendo wa nchi yao.

Amesema Serikali itaendelea kuimarisha miondombinu ya Skuli kwa kujenga skuli za kisasa ili Wanafunzi waweze kupata elimu itakayoweza kuwasaidia katika maisha yao na Taifa kwa ujumla.

Wakati huo huo amewataka wazazi na walezi kuacha kuwalaumu waalimu wakati watoto wao wanapofanya vibaya katika mitihani yao na badala yake wawe mstari wa mbele katika mbele sekta ya elimu.

kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Msingi Kisiwanduwi Ali Abdallah amewatak wanafunzi hao waliofaulu michipuo kutobweteka na badala yake wazidishe bidii katika masomo ili waweze kufikia malengo ya kupata elimu zaidi.

Nao baadhi ya Wanafunzi hao wameahidi kuendeleza kasi ya Masomo lengo la kupata wataalamu watakaoweza kuisaidia serikali kupata wataalamu wazalendo katika fani mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.