Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Azindua Kiwanda Cha Maji - Mkwawa Kilichopo Mjini Iringa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua kiwanda cha maji – Mkwawa  kilichopo mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu,Mama Mary Majaliwa, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Ali Happy, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda, Ahmed Huwel, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahnga, Naibu wa Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Iri ga, Richard Kassera
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha maji – Mkwawa, Ahmed Huwel  baada ya kuzindua kiwanda hicho mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahanga
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary  wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha maji-Mkwawa, Bw. Ahmed Huwel kuhusu ujazaji maji katika chupa wakati alipozindua kiwanda hicho mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Maji – Mkwawa, Bw. Ahmed Huwel kutembelea kiwanda baada ya Waziri Mkuu kuzindua kiwanda hicho mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha maji- Mkwawa, Bw. Ahmed Huwel (wa tatu kulia) kutembelea mitambo ya kuzalisha maji baada ya kuzindua kiwanda hicho mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege, wa pili kulia ni Mkuu wa mkoa  wa Iringa, Ally Happy na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahanga
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuzindua kiwanda cha maji- Mkwawa mjini Iringa, Septemba 25, 2019.
Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuzindua kiwanda cha maji – Mkwawa mjini Iringa, Septemba 25, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.