Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa Azindua Upanuzi wa Kituo cha Afya cha Idodi na Kuhutubia Mkutano wa Hadhara.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Ismani, William Lukuvi (wa tano kushoto) wakizindua Upanuzi wa Kituo cha Afya cha Idodi wilayani Iringa, Septemba 28, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM  Mkoa wa Iringa, Salim Abri, Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Naibu Waziri , Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege na kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Happiness Seneda.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Ismani, William Lukuvi baada ya kuzindua Upanuzi wa Kituo cha Afya Idodi wilayani Iringa , Septemba 28, 2019. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Upanuzi wa Kituo cha Afya cha Idodi Wilayani Iringa, Septemba 28, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Iringa, Costantino Kihwele, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahanga, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Ismani, William Lukuvi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Happiness Seneda, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wa Mkoa wa Iringa, Salim Abri, Mbunge wa Kalenga, Godfrey Mgimwa na Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa na Mkewe Mary wakimpongeza, Bibi Chipe Ngubi ambaye amejifungua mtoto wa kiume Greyson wakati walipozindua Upanuzi wa  Kituo cha Afya cha Idodi wilayani Iringa na kutembelea Wodi ya Mama na Mtoto, Septemba 28, 2019. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Ismani Wiliam Lukuvi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mkewe Mary wakitazama ngoma wakati walipowasili kwenye uwanja  wa kijiji cha  Idodi wilayani Iringa kuhutubia mkutano wa hadahara, Septemba 28, 2019. Wa tatu kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mandeleo ya Makazi, ambaye pia ni Mbunge wa Ismani, William Lukuvi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiwapungia wananchi wakati walipowasili kwenye uwanja wa kijiji cha  Idodi wilayani Iringa kuhutubia mkutano wa hadhara
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Ismani, William Lukuvi akiwasalimia wapiga kura wake kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Idodi wilayani Iringa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (aliyekaa wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkao wa Iringa na Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Idodi, Septemba 29, 2019. Kushoto (aliyekaa) ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mandeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Ismani, William Lukuvi.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.