Habari za Punde

Maonyesho makubwa ya sekta ya Kahawa kufanyika Zanzibar tarehe 30-31 Oktoba

 Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi  Amina Salum Ali akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusu mkutano wa maonyesho ya kahawa unaotarajiwa kufanyika Sea Cliff Mangapwani,huko katika ukumbi wa Wizara yake migombani 
Baadhi ya Waandishi wa vyombo mbali mbali  wakimsikiliza  Waziri wa Biashara na Viwanda Baloizi Amina Salum Ali  (hayupo pichani )  kuhusu mkutano wa maonyesho ya kahawa unaotarajiwa kufanyika Sea Cliff Mangapwani,huko katika ukumbi wa Wizara yake migombani .

PICHA NA KHADIJA KHAMIS MAELEZO ZANZIBAR  


Na Mwashungi Tahir       
Waziri wa Biashara na Viwanda Amina Salum Ali amesema Zanzibar imepata heshima kubwa  kwa kufanyika maonesho makubwa ya Sekta ya kahawa ambayo yanatarajiwa kufanyika  Sea Cliff Mangapwani ifikapo tarehe 31-31 mwezi huu.
Akizungumza na waandishi wa habari huko katika ukumbi wake wa mkutano  ulioko Migombani wakati akitoa taarifa kuhusu mkutano na Maonesho ya Kahawa “AFRICA SPECIALITY COFFEE EXPO 2019.
Amesema Zanzibar imepata fursa hii na itaweza kutangaza  sekta ya utalii kwani wageni wa mkutano huo watatembelea vivutio mbali mbali vya utalii , na kuweza kuongeza kipato .
Pia amesema fursa hiyo itaweza kuongeza ujuzi na utaalamu wa kuandaa kahawa za aina mbali mbali na pia kutoa nafasi za ajira kwa vijana baada ya hapo wataweza kujiajiri .
Aidha amesema utaalamu wa kuandaa kahawa za aina mbali mbali katika mahoteli makubwa ya kitalii kutaweza kupata ujuzi wa  kuandaa kahawa wenye kiwango kwenye mafunzo hayo waliobobea katika sekta ya kahawa.
Hata hivyo amesema lengo kuu la mkutano huo ni kuelimisha na kuonesha maendeleo ya masoko ya  kahawa pamoja na mikakati ya ndani na nje.
Vile vile wadau wa sekta hii wataonesha mashine za kisasa za kukausha , kusaga na kuandaa kahawa pamoja na vifungashio na maonesho haya yataweza kutatua changamoto ya mashine  na vifungashio vya kahawa.
Zaidi ya nchi 24 zimethibitisha kushiriki ambao ni wanachama wa jumuiya ya Nchi zinazozalisha kahawa miongoni mwao Ethiopia, USA, Brazilo, Colombia , Kenya , Italy,na baadhi ya nchi nyengine za kiarabu na Nigeria.
Waziri amina ametoa wito kwa wafanyabiashara wenye mahoteli wawekezaji katika sekya ya utalii na wananchi kutembelea maonesho hayo ili waweze kuona fursa mbali mbali.
Mkutano huo hufanyika kila mwaka kwa mzunguko kwa nchi wanachama ambapo kwa mara ya kwanza  Tanzania unatarajiwa kufanyika Zanzibar kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara na Viwanda,Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) na Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.