Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Afanya Ziara Maalum Kutembelea Miradi ya Maendeleo Wilaya ya Kaskazini "A"Unguja

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe kuashiria kuizundua Rasmi Gari ya Kubebea Wagonjwa ya Jimbo la Kijini iliyotolewa n mwakilishi wake Mheshimiwa Juma Makungu.

Na.Othman Khamis. OMPR.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitasita kumdhibiti mara moja Mtu au Kikundi chochote kinachoashiria kutaka kuiambukiza Jamii shari ya uvunjifu wa Amani hasa kipindi hichi ambacho Taifa linaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu Mwaka ujao wa 2020.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa indhari hiyo mapema wakati alipofanya ziara Maalum ya kukagua Miradi ya Maendeleo pamoja na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi inayosimamiwa na Taasisi za Serikali na Viongozi wa Majimbo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “A”.
Balozi Seif  Ali Iddi ambapo katika ziara hiyo alizindua Rasmi Gari la kubebewa Wajongwa iliyotolewa na Uongozi wa Jimbo la Kijini hapo Kituo cha Afya cha Kijini, kushiriki Kazi za Ujenzi wa Tawi la Kibuyuni Jimbo la Mkwajuni na kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa CCM Tawi la Chaani kubwa alisema Dola haitaridhia hata kidogo kuchezewa amani ya Nchi iliyopo.
Alisema hakuna Mwananchi hata Mmoja aliyeshiba Uzalendo na kulinda heshima  yake anayependelea kuona mazingira aliyoyazoea muda wote ya maisha yake yanazunguukwa na cheche za shari.
Alitahadharisha kwamba Wapo baadhi ya Watu wameshaanza harakati za kuzunguuka Mitaani Unguja na Pemba na kuanza cheche za fitna na majungu yanayoashiria kutaka kuwagawa Wananchi katika muelekeo wa Taifa kukaribia kuingia ndani ya Uchaguzi Mkuu Mwaka ujao.
Balozi Seif alisema wachafua Amani lazima waogopwe kwani ni sawa na Wagonjwa wa maradhi hatari ya kuambukiza kama kifua Kikuu wanaostahiki kudhibitiwa ili wasieneze uchafuzi huo na Serikali iko tayari kutekeleza udhibiti huo wa kulinda Amani ya Taifa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Viongozi wa Majimbo ya Wilaya ya Kaskazini “A” kwa kutekeleza vizuri Ahadi mbali mbali walizotoa kwa Wananchi wakati wakiomba ridhaa za kutaka kuwatumikia katika kipindi cha Miaka Mitano Majimbo yao.
Aliwataka Viongozi wa Majimbo mengine kuiga mfano wa Viongozi wa  Jimbo la Kijini uliojitolea kutoa msaada wa Gari la kuchukuliwa Wagonjwa kwa Wananchi wao lakini pia utaleta faraja kwa Majimbo yanayolizunguuka Jimbo hilo.
Alisema utekelezaji huo wa Ilani ya Uchaguzi nmdani ya Majimbo unakwenda sambamba na jitihada za Serikali katika kuimarisha huduma za Kijamii akitolea mfano Afya, Majio safi na salama pamoja na Miundombinu ya Mawasiliano yatakayopunguza usumbufu wa usafiri wa Wananchi hasa kusafirisha mazao yao kwa urahisi zaidi.
Balozi Seif alikariri kauli ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein iliyofafanua  utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi iliyofikia asilimia 85% ambao unaonyesha muelekeo wa Wananchi kuridhika nao ikiwa ishara ya kukubalika kuiamini CCM kupewa dhama ya kuendelea kuondoza Dola Mwaka 2020.
Alisema Serikali za Chama cha Mapinduzi zimeshafanya mambo mengi yanayopaswa kusemwa hadharani na kuacha tabia ya baadhi ya Watu kukebehi kila kitu.
“ Tuyaseme wenyewe maendeleo tuliyofikia tusiwaachie wengine wakatusemea. Bil shaka watatupotosha vibaya sana”. Alisem Balozi Seif.
Akigusia uendelezaji wa Miradi ya Chama Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM alisema uadilifu kwa Wanachama au Viongozi wanaopewa dhamana lazima usimame mwanzo ili  kufikia lengo lililokusudiwa.
Balozi Seif alisema wapo baadhi ya waliopewa dhama ya uendeleshaji huo hasa katika masuala ya fedha ambao hufikia wakati wakianzisha sintofahamu pale wanapotakiwa kutoa taarifa ya mwenendo wa Mapato yanavyokwenda.
Katika kuungua mkono harakati za kuendeleza Miradi na Majengo ya Chama cha Mapinduzi Balozi Seif aliahidi kuchangia Shilingi Milioni Moja kuongeza nguvu za Ujenzi wa Tawi la CCM Kubuyuni na Milioni Moja kwa Mradi wa CCM Tawi la Chaani Kubwa.
Mapema Mwakilishi wa Jimbo la Kijini Mheshimiwa Juma Makungu alisema katika Uongozi wake aliahidi kuendelea kuhudumia Matengenezo ya Gari hiyo ya kubebea Wagonjwa pamoja na Posho ya Dereva wa Gari hiyo.
Mh. Juma ambae pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati alisema hiyo ni miongoni mwa ahadi ya Gari Mbili alizotoa wakati wa Kampeni ya Uchaguzi ikiwemo ile ya mwanzo iliyokuwa ikitumika kwa shughuli za Kijamii pamoja na kuchukuliwa Wagonjwa.
Alisema gharama za vyombo hivyo vya Usafiri kwa ajili ya Wananchi wa Jimbo la Kijini pamoja na yale ya Jirani yanayolizunguuka viomegharimu jumla ya shilingi za Kitanzania Milioni 37,000,000/-.

Mheshimiwa Juma alisema kati ya hizo  Gari ya Kuchukulia Wagonjwa imegharimu Shilingi Milioni 23,000,000/- na ile ya huduma za Kijamii imegharimu Shilingi Milioni 14,000,000/-.

Balozi Seif  akimkabidhi Magamba ya Gari mbili za Jimbo la Kijini Mwenyekiti wa Jimbo hilo Nd. Wadi Juma Silima ikiwa ni Mali za Chama cha Mapinduzi.
Muonekano wa ndani ya Gari ya kubebea Wagonjwa ya Jimbo la Kijini itakayotoa huduma kwa Wananchi wa Jimbo hilo pamoja na wale wa Majimbo Jirani.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi akishiriki kazi ya Ujenzi wa Taifa katika Tawi la Chama cha Mapinduzi la Mbuyuni Jimbo la Mkwajuni.
Balozi Seif akiweka Jiwe a Msingi la Mradi wa Chama cha Mapinduzi Tawi la CCM Chaani Kubwa akiwa katika ziara ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM Wilaya ya Kaskazini “A”.Picha na – OMPR – ZNZ.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitasita kumdhibiti mara moja Mtu au Kikundi chochote kinachoashiria kutaka kuiambukiza Jamii shari ya uvunjifu wa Amani hasa kipindi hichi ambacho Taifa linaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu Mwaka ujao wa 2020.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa indhari hiyo mapema wakati alipofanya ziara Maalum ya kukagua Miradi ya Maendeleo pamoja na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi inayosimamiwa na Taasisi za Serikali na Viongozi wa Majimbo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “A”.
Balozi Seif  Ali Iddi ambapo katika ziara hiyo alizindua Rasmi Gari la kubebewa Wajongwa iliyotolewa na Uongozi wa Jimbo la Kijini hapo Kituo cha Afya cha Kijini, kushiriki Kazi za Ujenzi wa Tawi la Kibuyuni Jimbo la Mkwajuni na kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa CCM Tawi la Chaani kubwa alisema Dola haitaridhia hata kidogo kuchezewa amani ya Nchi iliyopo.
Alisema hakuna Mwananchi hata Mmoja aliyeshiba Uzalendo na kulinda heshima  yake anayependelea kuona mazingira aliyoyazoea muda wote ya maisha yake yanazunguukwa na cheche za shari.
Alitahadharisha kwamba Wapo baadhi ya Watu wameshaanza harakati za kuzunguuka Mitaani Unguja na Pemba na kuanza cheche za fitna na majungu yanayoashiria kutaka kuwagawa Wananchi katika muelekeo wa Taifa kukaribia kuingia ndani ya Uchaguzi Mkuu Mwaka ujao.
Balozi Seif alisema wachafua Amani lazima waogopwe kwani ni sawa na Wagonjwa wa maradhi hatari ya kuambukiza kama kifua Kikuu wanaostahiki kudhibitiwa ili wasieneze uchafuzi huo na Serikali iko tayari kutekeleza udhibiti huo wa kulinda Amani ya Taifa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Viongozi wa Majimbo ya Wilaya ya Kaskazini “A” kwa kutekeleza vizuri Ahadi mbali mbali walizotoa kwa Wananchi wakati wakiomba ridhaa za kutaka kuwatumikia katika kipindi cha Miaka Mitano Majimbo yao.
Aliwataka Viongozi wa Majimbo mengine kuiga mfano wa Viongozi wa  Jimbo la Kijini uliojitolea kutoa msaada wa Gari la kuchukuliwa Wagonjwa kwa Wananchi wao lakini pia utaleta faraja kwa Majimbo yanayolizunguuka Jimbo hilo.
Alisema utekelezaji huo wa Ilani ya Uchaguzi nmdani ya Majimbo unakwenda sambamba na jitihada za Serikali katika kuimarisha huduma za Kijamii akitolea mfano Afya, Majio safi na salama pamoja na Miundombinu ya Mawasiliano yatakayopunguza usumbufu wa usafiri wa Wananchi hasa kusafirisha mazao yao kwa urahisi zaidi.
Balozi Seif alikariri kauli ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein iliyofafanua  utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi iliyofikia asilimia 85% ambao unaonyesha muelekeo wa Wananchi kuridhika nao ikiwa ishara ya kukubalika kuiamini CCM kupewa dhama ya kuendelea kuondoza Dola Mwaka 2020.
Alisema Serikali za Chama cha Mapinduzi zimeshafanya mambo mengi yanayopaswa kusemwa hadharani na kuacha tabia ya baadhi ya Watu kukebehi kila kitu.
“ Tuyaseme wenyewe maendeleo tuliyofikia tusiwaachie wengine wakatusemea. Bil shaka watatupotosha vibaya sana”. Alisem Balozi Seif.
Akigusia uendelezaji wa Miradi ya Chama Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM alisema uadilifu kwa Wanachama au Viongozi wanaopewa dhamana lazima usimame mwanzo ili  kufikia lengo lililokusudiwa.
Balozi Seif alisema wapo baadhi ya waliopewa dhama ya uendeleshaji huo hasa katika masuala ya fedha ambao hufikia wakati wakianzisha sintofahamu pale wanapotakiwa kutoa taarifa ya mwenendo wa Mapato yanavyokwenda.
Katika kuungua mkono harakati za kuendeleza Miradi na Majengo ya Chama cha Mapinduzi Balozi Seif aliahidi kuchangia Shilingi Milioni Moja kuongeza nguvu za Ujenzi wa Tawi la CCM Kubuyuni na Milioni Moja kwa Mradi wa CCM Tawi la Chaani Kubwa.
Mapema Mwakilishi wa Jimbo la Kijini Mheshimiwa Juma Makungu alisema katika Uongozi wake aliahidi kuendelea kuhudumia Matengenezo ya Gari hiyo ya kubebea Wagonjwa pamoja na Posho ya Dereva wa Gari hiyo.
Mh. Juma ambae pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati alisema hiyo ni miongoni mwa ahadi ya Gari Mbili alizotoa wakati wa Kampeni ya Uchaguzi ikiwemo ile ya mwanzo iliyokuwa ikitumika kwa shughuli za Kijamii pamoja na kuchukuliwa Wagonjwa.
Alisema gharama za vyombo hivyo vya Usafiri kwa ajili ya Wananchi wa Jimbo la Kijini pamoja na yale ya Jirani yanayolizunguuka viomegharimu jumla ya shilingi za Kitanzania Milioni 37,000,000/-.
Mheshimiwa Juma alisema kati ya hizo  Gari ya Kuchukulia Wagonjwa imegharimu Shilingi Milioni 23,000,000/- na ile ya huduma za Kijamii imegharimu Shilingi Milioni 14,000,000/-.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.