Habari za Punde

Waajiri Wametakiwa Kuhakikisha Watumishi Wanashiriki Katika Michezo

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akifungua tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza leo jijini Dodoma ambapo kilele chake ni Novemba 14, 2019 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jahuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Mjaliwa. 

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma
Waajiri wametakiwa kuboresha mazingira ya kazi kwa kuhakikisha watumishi  wanashiriki  katika michezo na kufanya mazoezi  maeneo yao ya  kazi.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza leo wakati wa ufunguzi wa tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza linalofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ambapo kilele chake ni Novemba 14, 2019 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jahuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Mjaliwa.

“Mnaweza kuanzisha  timu  mbalimbali  za  michezo  na  kutenga  siku maalum katika mwezi kwa ajili ya mabonanza ya michezo kwa kuweka  mazingira  rafiki  ya  kufanyia  mazoezi kazini kwa kununua vifaa na kutenga vyumba vya mazoezi. Hii itaimarisha afya za watumishi na kupunguza gharama za matibabu katika taasisi husika.” Naibu Waziri Juliana Shonza.

Naibu Waziri Shonza amesema kuwa tamasha hilo linalenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika michezo mbalimbali na mazoezi ya viungo ili kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakiongezeka hapa nchini. 

Magonjwa yasioyoambukiza hutokana na  mitindo isiyofaa ya maisha kama matumizi  ya tumbaku, lishe duni, matumizi ya pombe kupita kiasi, pamoja na kutoshughulisha mwili au kutofanya mazoezi ya viungo mara kwa mara.

Magonjwa hayo ni kisukari, shinikizo la juu la damu, magonjwa  ya  moyo  na  mishipa,  saratani, pumu na magonjwa ya akili ambayo yamekuwa sugu na yana gharama kubwa za matibabu ambapo amesema kuwa watu  wengi hufikiria mazoezi ni lazima  ukimbie  au ucheze mpira, la hasha.Mazoezi ni jambo lolote linalohusisha misuli na kusababisha  kuongezeka  kwa  mapigo  ya  moyo  na  kasi  ya kupumua. 

Wataalam wa afya wanasema kuwa kiwango  cha mazoezi  kinacholeta  faida  ni  mazoezi yasiyopungua dakika 30 kwa  siku angalau siku tatu kwa wiki na  yanayomfanya  mtu kutokwa  na  jasho. 

Aidha, Naibu Waziri amesisitiza kuwa kupitia tamasha hilo, ufanyike uhamasishaji wa watu kupima afya hususani wa magonjwa yasiyoambukiza. Tiba ya mapema inapunguza uwezekano wa kupatwa na madhara zaidi. 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chemba Saimon Odunga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amewakaribisha washiriki wa tamasha hilo mkoani Dodoma ambalo limeshirikisha washiriki kutoka ndani na nje ya mkoa huo na hata nje ya nchi.

Odunga amewataka wakazi na wananchi wa mkoa wa Dodoma kutumia fursa ya tamasha hilo kwa kushiriki michezo mbalimbali hatua ambayo itwasaidia watu na jamii nzima kuweka afya zao katika hali bora ambayo inawatenga na magonjwa yasiyoambukiza.

Tamasha hilo ni la wiki moja ambalo limeandaliwa na kuratibiwa na Wizara  ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Sekretarieti  ya Mkoa wa Dodoma, pamoja na Wizara  ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ambapo limeshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, pete, kikapu pamoja mchezo wa kuvuta kamba. Tamasha hilo linaongozwa na kauli mbiu yetu ya mwaka huu; “Tutembee Pamoja Katika Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza” 
Katibu Mkuu Wazara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi (wa pili kushoto) akishiriki mazoezi  wakati wa ufunguzi wa tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza leo jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Naibu Katibu Mkuu (Afya) Dkt. Zainabu Chaula.
Watumishi wa Umma waliendelea na mazoezi mbalimbali leo uwanja wa Jamhuri Dodoma wakati wa ufunguzi wa tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza.
Watumishi wa Umma waliendelea na mazoezi mbalimbali leo uwanja wa Jamhuri Dodoma wakati wa ufunguzi wa tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza.  
(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma)
Venance Mwamoto Mbunge wa Kilolo ni akiendelea na mazoezi kabla ya ufunguzi wa tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza leo jijini Dodoma wakati timu ya Bunge akijiandaa na mchezo dhidi ya watumishi wa umma leo katika uwanja wa Jamhuri Dodoma. 
Katibu Mkuu Wazara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi (wa pili kushoto) akishiriki mazoezi  wakati wa ufunguzi wa tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza leo jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Naibu Katibu Mkuu (Afya) Dkt. Zainabu Chaula.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akito vifaa vya michezo mbalimbali wakatimwa ufunguzi wa tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza leo jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.